Juu
na chini ni Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongea machache
katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani katika kumuaga baada ya kumaliza ziara ya siku tano aliyofanya
Washington, DC na kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya
Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani lililofanyika
Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland.
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiingia Ubalozini kwenye chakula cha jioni
alichoandaliwa na Ubalozi huo kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya
kumaliza ziara yake ya siku tano.
Juu
na chini ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na maafisa na
wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC wakiwemo wanakamati wa
miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani/
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Sitti Mwinyi (watatu toka
kulia) wachukua chakula walichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani walipoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwaaga.
Afisa
Ubalozi Suleiman Saleh akitambulisha wakati mbele ya mgeni rasmi na
wageni waalikwa kwenye chakula hicho na kumtakia safari njema .
Mwenyekiti wa Kamati, Bwn. Baraka Daudi akijitambulisha kwa mgeni rasmi na kumtakia safari njema nyumbani.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi.
Rais
Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika
picha ya pamoja na Maafisa wakiwemo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Mama Sitti Mwinyi katika
picha ya pamoja na kamati ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la
Utamaduni wa Kiswahili Marekani.