JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
11 Julai, 2013
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa
kila tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya
kuwakumbuka mashujaa waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka
1978/1979.
Maadhimisho
hayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25
Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya
mashujaa yaliyopo Kaboya.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Sambamba
na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya
Ulinzi na Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi
mbalimbali za kiraia.
Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa Taifa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk