Rais
Goodluck Jonathan wa Nigeria amekutana na rais Xi Jinping wa China
mjini Beijing, katika ziara yake inayolenga kuimarisha uhusiano wa
kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Rais
Jonathan ambaye amefuatana na maafisa 19 wa ngazi ya juu wa serikali
yake, amesema China ina uchumi imara na kwamba kampuni za nchi hiyo
zinaendelea na mradi wa ujenzi wa barabara nchini Nigeria, wenye thamani
ya dola bilioni 1.7.
Wakati
wa mkutano huo, mikataba mitano ilisainiwa ikiwemo ya masuala ya
kibiashara, kanuni za visa, kiufundi na masuala ya kisheria
yanayohusisha kuuza na kununua bidhaa za kiutamaduni.
China
ambayo ina uchumi mkubwa barani Asia, imeonyesha nia ya kutaka kuongeza
maslahi zaidi katika sekta ya mafuta Nigeria, nchi ambayo inaongoza kwa
kuuza mafuta barani Afrika.