JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
PROGRAMU YA KUKUZA AJIRA KWA VIJANA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
PROGRAMU YA AJIRA
Programu hii itatekelezwa na Serikali kwa
kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini,Taasisi za fedha na wabia
wa maendeleo.Kwa kuanzia utekelezaji wake utaanza kwa kuendeleza
programu ya mfano iliyoanzishwa na Idara ya kilimo, uchumi na Biashara
katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye
kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya elimu ya juu katika kipindi
husika.
Kwa kuanzia serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanza utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa programu utakapoanza.
Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya
juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona
vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika
fani walizozisomea, tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji
na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa
programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji
na tathimini ya utekelezaji.
MADHUMUNI YA PROGRAMU.
Ni mojawapo ya hatua za utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 ya kuhamasisha uzalishaji wa
kitaifa
kufanikisha Ajira kamili yenye kipato na iliyochaguliwa kwa
uhuru,kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira na ajira isiyokidhi viwango
na kuongeza tija sehemu za kazi.
LENGO:
Lengo kuu la program ni kuongeza fursa za
Ajira 30,000 za moja kwa moja kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu kwa
kipindi cha miaka mitatu (3) na kuwawezesha vijana kujiajiri na hata
kuajiri vijana wengine kutokana na miradi watakayoibuni wao wenyewe.
Malengo mengine ni:-
1.Kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki shughuli rasmi za kiuchumi na wamejiajiri na kuajiri wengine.
2. Kukuza utamaduni wa kijasiriamali pamoja na ubunifu.
3.Kuhamasisha matumizi bora ya nguvu kazi.
PROGRAMU INALENGA.
Programu hii inalenga vijana wa elimu
ya juu ambao wapo tayari kuanzisha shughuli za kujiajiri katika sekta
ya kilimo cha mazao, ufugaji, uvuvi, misitu na usindikaji.
MIRADI.
Miradi itakayoanzishwa itatoa ‘Mnyororo mzima wa thamani’ au INTERGRATED CROSS VALUE CHAIN (ICVC)
Kwa mfano,mradi wa Alizeti na ukamuaji mafuta.
1st step- Uandaaji mashamba,ulimaji,upandaji,palizi na uvunaji
2nd step- Usafirishaji, uhifadhi, usindikaji
3rd step- Ukamuaji mafuta, ufungashaji na uuzaji mafuta.
MAHITAJI YA RASILIMALI.
Jumla ya shilingi bilioni 54.451
zitahitajika kwa kipindi cha miaka 3 ya utekelezaji wa programu ambapo
shilingi Bilioni 50 zitawekwa dhamana na shilingi bilioni 4.451
zitatumika katika mafunzo na kuwaandaa vijana ili waweze kukopesheka
MATOKEO YA PROGRAMU HII.
I. Vijana watajengewa uwezo wa
kujiajiri katika sekta zilizotajwa za kilimo, usindikaji, uvuvi na
maeneo mengine kama vile viwanda vidogo na vya kati.
II. Kuongezeka kwa fursa za Ajira nchini na kupungua kwa kiwango cha umaskini.
III. Kupungua kwa matukio ya uhalifu na vitendo visivyokubalika katika jamii.
IV. Kupungua kwa kasi ya vijana kuhamia mjini na kuimarika kwa uchumi wa nchi.
MATOKEO TARAJIWA YA PROGRAMU.
Programu hii ya wahitimu wa elimu ya
juu itatoa fursa za Ajira kwa wahitimu 30,000 kutokana na miradi 1,000
kwa kipindi cha miaka 3.
Uzoefu unaonesha kuwa mradi mmoja wa kilimo wenye thamani ya sh. milioni 50 una uwezo wa kutoa ajira kwa wahitimu 20 hadi 30.
PROGRAMU ITATEKELEZA KATIKA AWAMU 3.
(a) Awamu ya kwanza itahusisha vijana
wahitimu 600 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) kumiliki miradi 200
ya kujiajiri na kuajiri wahitimu wengine wasiopungua 5,400 kutoka maeneo
mengine.
(b) Awamu ya pili imelenga
kuwawezesha vijana 900 wa elimu ya juu kutoka vyuo vingine ambao watakua
tayari kuanzisha miradi ya kujiajiri na kuajiri wengine .Ambapo Miradi
300 itawezesha kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa vijana wahitimu
wasiopungua 8,100.Hapa miradi itahusisha sekta nyingine zitakazoonekana
zina tija na kuongeza fursa za ajira.
(c) Awamu ya tatu imelenga
kuwawezesha vijana wahitimu 1,500 wa vyuo mbalimbali vya kati vikiwepo
vya VETA. Jumla ya miradi 500 itawezeshwa na kuzalisha ajira kwa vijana
13,500.
PROGRAMU ITAJUMUISHA YAFUATAYO.
I. Utambuzi na uhamasishaji vijana—ambapowataandikishwa kupitia mikoa na Wilaya wanayoishi
II. Kutoa mafunzo ya ujasiria mali
na stadi zakazi-mafunzo yatatolewana SUA,baadae kwani kubuni na kuandaa
andiko la Biashara (Business proposal)
III. Kujenga uwezo wa vijana
kulingana na miradi waliyoainisha –lengo ni kuwapatia ujuzi na uzoefuwa
namna ya utekelezaji miradi.
IV. Mafunzo na uzoefu kwa
waendeshaji wa program-Wahusika watajengewa uwezo kujifunza kutokana na
miradi ya ukuzaji ajira katika nchi nyingine.Taasisi husika Wizara ya
Kazi na Ajira,Benki ya CRDB,SUA na SUGECO.
V. Kutoa mafunzona huduma za kitaalamu na uratibu katika maeneo ya uzalishaji.
UTARATIBU WA UKOPESHAJI.
v Program hii ni ya miaka 3 na mikopo itakayotolewa ni ya miaka 3 na urejeshwaji wa mikopo ni kuanzia miaka3 hadi 5.
v Muda wa mkopaji kurejesha mkopo ni kuanzia miezi 6 hadi mwaka 1 kutegemeana na aina ya mradi.
v Utaratibu wa ukopeshaji ni wastani wa sh. mil 50 hadi 300mil kulingana na mradi.
Utaratibu wa utekelezaji na viwango vya riba utaainishwa katika mpango kazi wa utekelezaji programu