Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, July 17, 2013

Picha za M2theP akiwa kwenye XXL ya CloudsFM, isikilize pia single yake mpya

.
M2theP
Kwa mara ya kwanza toka kitokee kifo cha rapper Albert Mangweha (Ngwair) rafiki yake wa karibu ambae ni M2TheP waliekua pamoja Afrika Kusini mpaka umauti umemkuta Ngwair, amefanya interview kwa mara ya kwanza kwenye radio kupitia XXL ya @CloudsFM na kuzungumza machache pamoja na kutambulisha single yake mpya na ya kwanza toka kifo kitokee.
M alishindwa kujibu maswali mengi yaliyotaka kujua kilichotokea kwa Ngwair na akaishia tu kukanusha kuhusu ishu za dawa za kulevya kwa kusema sio kweli kwa sababu siku zote dawa za kulevya huwa hazichukuliwi South zikaletwa Tanzania bali huchukuliwa Tanzania na kupelekwa South Afrika.
Akiwa bado anajisikia uchungu kwa kile kilichotokea kwa Ngwea, M2theP alishindwa kueleza kuanzia mwanzo mpaka mwisho lakini akaahidi kukisema vyote siku chache zijazo mbele ya Waandishi wa habari.
2
.
Dj Zerro, M na B12
.
Adam Mchomvu na M
.
Adam Mchomvu, M, Dj Fetty na B12

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...