Mchezo unazidi kuwa mgumu kadri siku zinavyozidi kwenda sababu idadi ya
wanaopaswa kuendelea na mchezo ndivyo inavyohitajika kuwa ndogo mpaka
siku ya 91 atakapobaki mtu mmoja wa kukabidhiwa $300,000 kama zawadi ya
BBA The Chase.
Nominations za wiki hii zimewagusa baadhi ya washiriki ambao hawajawahi
kabisa kupendekezwa kutoka, na wengine ambao wameshawahi kupendekezwa
mara moja na zaidi lakini waliokolewa na kura za watazamaji.
Baada ya kupona kutoka wiki iliyopita na kuwa HOH , cheo kilichompa
nafasi ya kujiokoa katika nomination zilizopita Nando wa Tanzania
ameungana na washiriki wengine 6 katika orodha ya majina yaliyotajwa na
Biggie kuingia katika kikaango cha eviction ya wiki hii.
Washiriki ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika nominations za wiki
hii ni pamoja na aliyekuwa kipenzi cha Huddah mjengoni, Angelo wa Afrika
Kusini ambaye amewekwa na HOH wa wiki hii Elikem aliyejiokoa na nafasi
yake kumuwekea yeye.
Fatima wa Malawi, Bimp wa Ethiopia pamoja na Cleo wa Zambia ndio
washiriki wengine ambao wameingia dangerzone kwa mara ya kwanza toka
mchezo umeanza.
Washiriki ambao waliwahi kupendekezwa na kuokolewa na kura za watazamaji
na wameingia tena wiki hii ni pamoja na Pokello wa Zimbabwe, Hakeem wa
Zimbabwe pamoja na Nando wa Tanzania.
Wiki hii Ghana na Nigeria ndio zimekalia viti vya utawala wa nyumba, Ruby ikiongozwa na Elikem na Melvin akiiongoza Diamond.
Kura yako inahitajika kumwokoa Nando ili aendelee kubaki na kuiwakilisha
Tanzania katika msimu wa 8 wa BBA The Chase unaoendelea Afrika Kusini.