Hapa ni wakati Jokate alipoamua kukaa na Mpeka kistaarabu kuongea nae kabla ya hatua za kisheria
Message alizotumia watu kwenye facebook na msg za simu za mkononi.
Aliyefanikisha huyu jamaa kukamatwa ni mrembo mmoja model Blessing ambae alishiriki Miss Morogoro 2013 ambapo namkariri akisema:
“Wiki mbili zilizopita nilipata msg kwamba Kidoti hair na Mzinga Planet
wanahitaji mamodo kwa ajili ya kutengeneza matangazo kwa ajili ya nywele
za kidoti, tulikua Morogoro kwa ajili ya Miss Morogoro tukaja Dar mpaka
Mzalendo Pub msg ilipotuelekeza lakini nilivyoingia sikuona mtu ambae
anahusiana na Jokate, niliona watu ambao nawajua lakini sio kuhusu
nywele.
"Nikampigia kaka mmoja anaitwa Johnson kwa sababu najua anafahamiana na
Jokate, nikampigia kumfokea kumwambia nyinyi vipi mbona mmetangaza
audition alafu sioni hata mtu mmoja ambae anahusika? naona watu ambao
kampuni zao zipo majumbani kwao?
"Baada ya dakika zaidi ya 10 kina Jokate wakawa wameshafika japo baadhi
ya mamodo wengine walikua wameshaondoka lakini baadhi ya viongozi kama
Majaji wa kike walikuwepo na walipoulizwa wakasema tumsubiri Mpeka ambae
ndio muhusika na pia Mkurugenzi wa Mzinga Planet” – Blessing
Baada ya kina Jokate kufika Mpeka alipigiwa simu ili arudi Mzalendo Pub,
japo alisita sana mtuhumiwa huyu alikuja kwenye eneo la tukio na
kukutana uso kwa uso na Jokate na timu yake, baada ya hapo akaanza
kusingizia kwamba yeye hahuusiki ila kuna watu wengine ndio wanahusika
ila alipotoa namba zao wakapigiwa simu, kila mmoja alionekana kutaharuki
kwa sababu hawajui chochote kuhusu hiyo Mzinga Planet.
Baada ya Jokate na timu yake kukaa na Mpeka na kumuuliza kistaarabu bila
kutoa ushirikiano wa kutosha, uamuzi ulitoka kwamba apelekwe Polisi
Osterbay ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.
Mpeka alikua anaonekana analia wakati mwingie na hiyo ilikua ni baada ya
kumpiga huyu msichana shuhuda aitwae Blessing kwa sababu alimchomea
mpaka akakamtwa.
Credti: Millard Ayo