Jeshi
la polisi mkoani Kilimanjaro linamhoji mkazi mmoja wa mjini Moshi
kufuatia kisa cha mtoto wake kutoweka nyumbani na silaha anayoimiliki
kihalali.
Bwana
Antony Justine mkazi wa kiboroloni mjini Moshi ambaye ni ni mmilikiki
halali wa silaha aina ya bastola yenye nambari PA 21738 V anadaiwa
kuhifadhi silaha hiyo kizembe kiasi cha kusababisha mtoto wake kuiba
silaha hiyo.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro Roberty Boaz amesema katika mkutano wake
na waandishi wa habari kuwa silaha hiyo ilichukuliwa na mtoto wa familia
ya Bwana Antony aitwaye Melkzedeck 23.
Mtoto
huyo alichukua silaha hiyo na vifaa vingine kisha kuisalimisha kwa
polisi baada ya kutoa shinikizo kuwa asibughudhiwe vinginevyo atajiua
kwa kutumia silaha hiyo.
Hata
hivyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wasamaria wema limefanikiwa
kuioka silaha hiyo kutoka mikononi kwa kijana huyo lakini halikufanikiwa
kumkamata kwani aliiacha silaha kichakani na kutokomea kusikojulikana.
Kisa
hicho bado kinaumiza vichwa vya maafisa wa polisi na hadi sasa
uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika kubaini chanzo cha tukio hilo.
Kamanda
Boaz amesema jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa mmliki wa silaha
hiyo bwana Antony kwa uzembe wa kuhifadhi basatola yake huku likitoa
mwito kwa wamiliki wengine wa silaha kuwa makini katika utunzaji wake
vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.