Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo
Mtoto
aliyefahamika kwa jina la Lina Krisantus(4), amefariki baada ya
kugongwa na gari wakati akivuka barabara katika maeneo ya Tegeta kwa
ndevu jijini Dar es Salaam.
Akidhibitisha
kutokea kwa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
Camillious Wambura, alisema mtoto huyo alifariki baada ya kugongwa na
gari lenye namba T 670 ANF aina ya Benz lililokuwa likitokea Tegeta
Kibaoni kuelekea darajani.
Alisema
dereva wa gari hilo hakuweza kufahamika kwani alikimbia baada ya ajali
na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyama na juhudi za
kumsaka dereva huyo zinaendelea.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Aidha,
katika tukio lingine moto umeteketeza nyumba ya vyumba kumi na vyoo
viwili pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani ya nyumba hiyo, zenye
thamani ya Sh milioni 15 juzi jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema nyumba hiyo iliyoko
maeneo ya Kigamboni Southen Beach ambamo wanaishi wafanyakazi wa
kampuni hiyo, iliteketea majira ya saa 9.
Alisema
chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni moto uliokuwa umewashwa kwa ajili
ya kuchoma taka na moto huo kusambazwa na upepo na kusababisha cheche
zilizoruka kwenye paa la nyumba hiyo na kuiteketeza ingawa hakuna
madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu.
CHANZO: NIPASHE