Rais wa Misri Mohammed Morsi
amesisitiza kwamba yeye ndiye kiongozi halali wa taifa huku maandamano
kati ya wapinzani na wafuasi wake yakisababisha vifo zaidi.
Kwenye hotuba aliyotoa kwa taifa usiku wa
kuamkia leo, Mosri alipinga makataa ya jeshi kutatua mgogoro wa sasa
ifikapo Jumanne. Kiongozi huyo amesema hataamrishwa na yeyote na
kuwasihi waandamanaji kuweka utulivu.Hata hivyo watu 16 walikufa katika moja wapo ya maandamano ya wafuasi wa Morsi. Awali jeshi lilitoa mpango wa kurejesha taifa katika uthabiti.
Stakabathi iliyopatikana na BBC inasema jeshi linapanga kuvunja katiba, kuweka mchakato wa uchaguzi mkuu, na kuvunja bunge.
Hapo Jumatatu Jeshi lilisema huenda likaingilia kati ikiwa hali haitabadilika. Morsi na wanasiasa walipewa saa 48 kuafikiana.
Chanzo: BBC



