Mlezi
wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha
Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam, leo Julai 6, 2013.
Mlezi
wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe.
Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, leo Julai 6, 2013 kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao.
Baadhi
ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa
katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
alipozungumza nao leo.
Baadhi
ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama
kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
alipofika ukumbini hapo kuzungumza nao leo, Julai 6, 2013. Picha na OMR