Mhubiri
Raia wa Uganda Richard Mwangusi akiwa chini ya ulinzi wa polisi
usiku huu baada ya kutuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kupitia huduma ya M-PESA
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Ramadhan Mungi akitoa kituo cha
polisi mjini Iringa ambako mhubiri huyu anashikiliwa na jeshi la
polisi kufuatia wananchi kulalamika kufanyiwa vitendo vya kitapeli na
mhubiri huyo ,kamanda Mungi amekuwa ni mmoja kati ya makamanda wa
mfano nchini kutoka na kufanya kazi usiku na mchana na kuwa jirani
zaidi na askari wake
Kikosi
cha kazi cha jeshi la polisi mkoa wa Iringa wakiwa njeya kituo
cha polisi ambako mhubiri huyo anashikiliwa usiku huu kwa tuhuma za
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
KILIO cha wengi kuhusiana na
vitendo vya utapeli vinavyofanywa na baadhi ya wahubiri ambao
wamekuwa wakijitafutia fedha kupitia injili hapa nchini ,kimeanza
kusikilizwa baada ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumkamata na
kumtupa mahabusu mhubiri Richard Mwangusi ambae ni raia wa nchini
uganda kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mapema leo kupitia mitandao mbali
mbali ya kijamii baadhi ya wasamaria wema wameeleza kusikitishwa na
kito cha utapeli kinachofanywa na mhubiri huyo ambae amekuwa
akiishi katika nyumba moja ya kulala wageni ya Wihanzi mjini Iringa
kuwa amekuwa akiwataka watu mbali mbali kutuma pesa kwa njia ya
M-PESA kuanzia kiasi cha kati ya TSh 10,000 na kuendelea iwapo
wanahitaji kupanga muda wa kuongea na mhubiri huyo kupitia simu ya
kiganjani



