Na Bazil Makungu Ludewa
TAASISI
ya kuzuia na kupambana rushwa wilayani Ludewa (Takukuru) imempandisha
kizimbani mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Atanasio
Munge kwa makosa ya ubadhilifu wa jumla ya shilingi 4.2 milioni mali ya
halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbele ya hakimu mkazi mheshimiwa JUMA HASSANI katika
mahakama ya mkoa Iringa mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa Imani Mitume akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa
anakabililiwa na makosa manne ikiwemo matumizi ya nyaraka kosa
linaloangukia kwenye kifungu namba 22 ya sheria ya kuzuiaz na kupambana
na rushwa namba 11/2007.
Makosa
mengine ni ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma chini ya namba 28(2)
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na 11 ya mwaka 2007, kosa
lingine ni kuibabishia hasara serikali shilingi milioni 4 makosa chini
ya kifungu namba 10(1) jedwari la 57(1) na jedwari la 60(2).
Pamoja
na mhandisi Atanasio Munge mshtakiwa wa pili ni mfanyabiashara wa
mgahawa Videa Kayombo maarufu kama (mama hadija) ambaye jina,saini na
mgahawa wake vilitumika kutoa stakadhi zinazoonesha kuwa alitoa huduma
hewa ya chakula chenye thamani ya shilingi m.4.2 kwa wananchi wa
vijijini katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji wilayani Ludewa
inayofadhiriwa na Benki ya dunia.
Akisoma
hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa (TAKUKURU) Imani Mitume alisema watuhumiwa wote wawili
walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2010 na 2012 na kwamba Vedea Kayombo
alitoa risiti za uongo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Kufuatia
tukio hilo Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
Edings Mwakambonja ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kutoa
ushirikiano na ofisi yake kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa lakini
pia akawahimiza kusimamia miradi inayopelekwa na serikali katika maeneo
yao.
Mwakambonja
pia amewataka watumishi wa umma kuwa waadlilifu katika kazi zao ili
kuiepushia serikali hasara na kusababisha kuzorota kwa huduma bora za
kijamii jambo linalosababishwa na watumishi wasio na uzalendo na nchi
yao.