Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema ikiwa mafisadi
hawatadhibitiwa, iko hatari wakajiimarisha kufikia hatua ya kuiongoza
nchi siku zijazo.
Dk. Mengi alitoa kauli hiyo jana kwenye kongamano la siku moja baina ya serikali, taasisi za serikali na wafanyabiashara, lililokwenda sambamba na uzinduzi wa ripoti mtazamo wa viongozi wa biashara kuhusu mazingira ya uwekezaji Tanzania mwaka 2013.
“Wala rushwa wakubwa ni kina nani na wako wangapi? Ukiniuliza mimi nitakwambia hawazidi wanne, wanafahamikaila sitawataja kwa leo,” alibainisha.
Dk. Mengi alitoa kauli hiyo jana kwenye kongamano la siku moja baina ya serikali, taasisi za serikali na wafanyabiashara, lililokwenda sambamba na uzinduzi wa ripoti mtazamo wa viongozi wa biashara kuhusu mazingira ya uwekezaji Tanzania mwaka 2013.
“Wala rushwa wakubwa ni kina nani na wako wangapi? Ukiniuliza mimi nitakwambia hawazidi wanne, wanafahamikaila sitawataja kwa leo,” alibainisha.
Alisema rushwa kubwa ipo nchini na tuendako
ana wasiwasi kuwa wala rushwa wakubwa ndiyo watatawala nchi kupitia
matakwa yao kwa nchi kuongozwa na kutawaliwa na watu wasioonekana wala
kujulikana.
“Ni watu wenye nguvu wanajipenyeza hadi katika vyombo vya dola, mtu anaweza kupoteza kazi kwa uamuzi wao,” alisema.
Dk. Mengi aliongeza kuwa wapo wanaosema
tatizo la rushwa litamalizwa kwa utashi wa kisiasa, lakini hauwezi
kufanikiwa kama hakuna utekelezaji na kutambua kuwa rushwa kubwa
inateketeza Taifa.
Alisema kuna sababu nne zinazosababisha
mafisadi wasishughulikiwe ikiwamo kuogopwa kwa kuwa wana nguvu za
kuwadhuru wanaowashughulikia, mlolongo wa utoaji rushwa na kuna
wanaonufaika na ndiyo wanaotakiwa kuwashughulikia na kukosekana kwa
ujasiri wa kuwashughulikia.
Dk. Mengi alibainisha kuwa wala rushwa
wakubwa hapa nchini wako wanne na wanafahamika lakini kutokana na sababu
mbalimbali ikiwamo kuogopwa, wameendelea kutafuna mali ya umma bila
woga wowote.
Alisema ripoti ya hivi karibuni ya masuala
ya rushwa iliyotolewa na Shirika la Transparence International,
imeonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 14 kwa rushwa, hali ambayo
inatisha.
Alisema matokeo ya rushwa ni mabaya kwa watu maskini kwani ni wizi wa kumwibia mvuja jasho.
Mengi alisema wapo wanaosema kuwa yeye
(Mengi), si mwathirika wa rushwa lakini ukweli ni kwamba alipoteza
miradi mikubwa miwili kutokana na kukataa kutoa rushwa.
“Sitataja kuwa miradi yangu ilipotea katika
awamu ipi ya serikali, lakini sijakata tamaa na sitaogopa nitaendelea
kuzungumzia na kupambana na rushwa,” alisema.
Alisema haiwezekani kuendesha nchi kwa
misingi ya rushwa, hivyo ifike mahali Taifa likubali kutengana nayo na
kuwatenga wala rushwa wakubwa na wadogo, lakini kuendelea kuwakumbatia
Taifa litaanguka.
Alisema Taifa linakabiliwa na tatizo la
uwapo wa watu wasiofahamu kitu kujinadi kuwa ndiyo wanafahamu na
kuhusika katika maamuzi ya kupanga kodi kwa wafanyabiashara.
Alisema kwa sasa anafanya sala Taifa lisifike mahali mafisadi kutawala na kuachwa wafanye watakavyo.
Aidha, alisema kuna uhusiano mkubwa kati ya wala rushwa wakubwa na mtandao wa biashara ya dawa za kulevya.
Alisema biashara ya dawa za kulevya inakua na vijana ndiyo wanatumika katika biashara hiyo.
“Huwezi kutenganisha biashara ya dawa za
kulevya na wala rushwa wakubwa, hawa ndiyo wafanyabiashara wa dawa za
kulevya, wanawatumia vijana kufanikisha biashara zao,” alisema.
“Vijana na wasanii wetu wanatumika katika
biashara hii, waliokamatwa Afrika Kusini si rahisi wawe na kiasi hicho
cha fedha, bila ufadhili wa wala rushwa wakubwa, aliyewatuma si mtu
mdogo bali mla rushwa mkubwa,” alisema Dk. Mengi.
Aidha, alisema vijana ndiyo tegemeo la
Taifa na wateja wa bidhaa zinazouzwa na wafanyabiashara, hivyo upo
wajibu mkubwa wa kupinga kwa vitendo suala la rushwa.
Alisema ni lazima Watanzania wachukue hatua
za kukabiliana na wala rushwa na lawama kubwa ni kwa Watanzania ambao
wanashindwa kuwaunga mkono wanaopinga rushwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania, Godfrey Simbeye, alisema ripoti iliyozinduliwa ilijikita
katika kuangalia mazingira ya uwekezaji Tanzania na kubainisha mambo
yanayokwamisha uendeshaji na ukuaji wa biashara nchini.
Alisema wengi wa wafanyabiashara
waliohojiwa waliainisha vikwazo kuwa ni ukosefu wa umeme, kiwango cha
kodi, rushwa na mrundikano wa kodi.