NAKUMBUKA
muziki wa kizazi kipya ‘Bongo fleva’ ulivyotoka mbali, tangu enzi za
Gangwe Mob, Sugu akiitwa ‘2 Proud’, Big Dog Pose, Hard Blasters, Balozi
Dolar Soul, Mr Paul na wengine wengi sana ambao walikuwa wakighani na
kuimba kipindi hicho.
Ni
ukweli usiopingika kuwa wanamuziki walioanza kuimba kipindi hicho
walipata shida sana kwa kuimba pasipo kujua kuwa muziki wanaoutengeneza
ni pesa, lakini inakosa thamani kutokana na uelewa duni wa mashabiki
ambao walikuwa bado hawajaukubali.
Katika
harakati zao za kimuziki, wasanii hao waliweza kuimba bure kwa kipindi
chote hicho na hata wale waliofanikiwa kutoa albamu hawakuweza kuuza kwa
kiwango kile kinachofikiriwa.
Hiyo
ilitokana kuwa wapenzi wengi wa muziki kwa kipindi hicho walikuwa ni
wale wasio na kazi na watoto wa mama ambao wanakaa nyumbani na kutoka
mashuleni.
Lakini
hali ilibadilika kwa kipindi cha miaka ya tisini mwishoni na mwanzoni
mwa mwaka 2000, ambapo Niger Jay (Prof Jay) alifanikiwa kubadilisha
mtazamo wa wanajamii.
Chemsha
bongo ndio ilikuwa nyimbo ambayo inatamba sana akiwa na kundi la Hard
Blasters, ambalo lilikuja kuwa tishio kwa muda mfupi na kupotea.
Jay
mara baada ya kutoa wimbo huo ndio ukaweza kubadilisha mtazamo na
kuongeza mashabiki wa kila rika katika muziki wa bongo fleva.
Mara baada ya wimbo huo ndipo mapinduzi ya muziki pesa yakaja katika muziki huu bongo fleva.
Kipindi
cha mapinduzi hayo maproduza waliweza kufaidika sana kwa kuwapa wasanii
lebo ya kurekodi bure kisha kugawana fedha za albamu.
Wasanii walipunjwa sana kipindi hicho na Wahindi kutokana na uelewa mdogo wa soko juu ya suala la muziki.
Lakini ilipofika hatua wakagundua kuwa wananyonywa kila msanii aligoma kutoa albamu na kuanza kuimba nyimbo moja moja.
Nyimbo hizo zilifanya vizuri katika soko na kuwapatia fedha nyingi za kutosha kupitia shoo mbalimbali walizokuwa wanafanya.
Mapinduzi
ya kutegemea shoo yamekua sasa mpaka hatua ya kuwa na video bora katika
luninga zetu kiasi cha kufikiria soko la Magharibi.
Hali
hiyo imekwenda sasa kwa wasanii hao kuacha tena kufikiria muziki na
baadaye kugeuka ni watu wa kutumiwa na wajanja wa mjini kutokana na
majina yao.
Wasanii
wengi wamekuwa vishoka vya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na
kutamani kuwa na pesa nyingi kiasi cha kujiingiza katika biashara hiyo
haramu.
Hili
limebainika kutokana na kuamini kuwa majina yao makubwa yanahitaji pesa
nyingi za matanuzi, hivyo wasipokuwa nazo wataaibika.
Jambo ambalo nawaambia si kweli bali wanachotakiwa kutengeneza mazingira mazuri kwenye muziki wao ili wafanikiwe.
Nawashauri
wasanii wa muziki huu wa kizazi kipya kutumia vizuri mapato yao ambayo
wanapata kwa sasa ili kujijengea maisha yao ya baadaye.
Kwani
kushinda baa kila siku na kutembelea magari makubwa ya kuazima kwa
gharama kubwa si ujanja, bali wanatakiwa kuangalia wapi wataongeza
masoko yao ya sanaa.
0716 -772231
MTANZANIA
MTANZANIA