MAPENZI NI HATAREE:: WAKUTWA NA MAUTI WAKIFANYA MAPENZI. SOMA HAPA
Kwa Mujibu wa
Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw.
Mathias Nwoko,45, na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti
wakati wakiwa katika tendo la ndoa.Wawili
hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa
furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao,
Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13
bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea
kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.Mathias
alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi
amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku
unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi
ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.Mpaka
asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote
mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao
ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa
juu ya mwanaume.Aliganda
kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo
kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa
taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye
alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise.