Kijana
ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja (mwenye t-shirt
nyeupe) akiwa mikononi mwa vijana wasamalia mwema waliomkamata katika
moja ya mabanda ya maonyesho ya sabasaba akikwapua simu katika banda
hilo huku akiwa ameharibika usoni baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi
na raia wenye asila kali
Kijana
ambaye alikamatwa akiiba simu katika moja ya banda lililopo kwenye
maonyesho ya Sabasaba Akiwa amepigwa tanganyika jeki huku akiwa
kashapokea kipigo cha mbwa mwizi baada ya kukamatwa na raia wenye asila
kali katika viwanja hivyo hapo jana
Kibaka
akiwa kwenye mikono ya mwana usalama wa JKT akipelekwa katika Kituo Cha
Polisi Cha Sabasaba Mara baada ya kupokea Kichapo Kutoka Kwa Raia wenye
asila kali katika viwanja vya sabasaba hapo jana
Kijana
ambaye hakufahamika jina lake alijikuta kwenye wakati mgumu sana leo
mara baada ya kumrushia makonde askari wa jeshi la kujenga Taifa (JKT)
katika maonyesho ya Sabasaba baada ya kutaka kumzuia askari huyo
asifanye kazi yake wakati akitaka kumkamata mwizi. Baada ya Raia
kujikuta wakitoa kipondo kwa kijana ambaye aliiba simu ndipo askari huyo
aalipotokea na kutaka kumkamata lakini jamaa huyo akishikwa na polisi
hapo juu katika picha laitokea na kutaka kumzuia askari huyo asifanye
kazi yake vizuri ndipo ukaanza ubishani na hapo ndipo ngumi zikaanza.
Baada ya Askari huyo kutumia Vyema mafunzo aliyopewa kambini wakati
wakujiunga na Jeshi hilo ndipo alipoweza kumtia nguvuni na bila ubishi
akaingia kwenye kumi na nane za askari.
Jamaa akiwa mpole huku akipelekwa kituoni tayari kwa maamuzi mengine
Taratibu akipelekwa kituo cha Polisi tayari kwa hatua zaidi kuchukuliwa
CREDITS": LUKAZA BLOG