IGP Sais Mwema
Kagera.
Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameteka mabasi mawili ya
abiria na kufanya uporaji katika Pori la Hifadhi ya Biharamulo Mkoani
Kagera na kupora bunduki aina ya SMG iliyokuwa na askaRi aliyekuwa
anasindikiza mabasi hayo.
Akithibitisha
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema
majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya
Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika
majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.
Kwa
mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS lililokuwa likielekea
Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es Salaam,ambapo kabla waliteka
gari dogo na kulitumia kufunga barabara katika hali iliyoonekana
lilikuwa limeharibika.
Katika
tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Rugaihura
(47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa shingoni kwa risasi, ambapo
majambazi hao walipora mali mbalimbali za abiria zikiwemo fedha na simu.
MWANANCHI