Elizabeth Michael ‘Lulu’
MUIGIZAJI
machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya
kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala
kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. Lulu alisema hayo juzi, katika
kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha
Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.
“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.
“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini
yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja
kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.
Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo
fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha
kuzisikiliza.
MTANZANIA