Wananchi
waliowengi wanakubaliana na hoja za Mzee Bomani kwamba mifumo miwili, ya
Serikali moja,mbili haina nafasi kwenye kizazi cha leo na hata cha
baadae.
Kimsingi,mfumo
wa Serikali mbili umethibitisha udhaifu katika utekelezaji wake na
Watanzania hususan Wazanzibari sasa wanauzoefu wa miaka hamsini ya
mazonge ya mfumo huo uliozalisha kero za Muungano.
Jaji
Bomani amesema kwamba kwa mtazamo wake, mfumo wa kuwa na Serikali tatu
ndio muafaka. “Mfumo wa Serikali moja hauna uwezekano…ili lilibainisha
miaka 50 iliyopita,mfumo wa Serikali ndio hivyo tumejionea matatizo na
kero zake na ubishi usiokwisha”.
Naam, zimeundwa Tume na
Kamati
zilizoongozwa na Majaji na watu wenye kuheshimika hapa nchini kuangalia
utatuzi wa kero za Muungano,lakini hazikuweza kuzaa matunda,malalamiko
yamezidi katika kila upande wa Muungano huu,Zanzibar na Tanganyika.
Bila
shaka wengi wanakubali dhana ya mfumo wa Serikali tatu katika Muungano
wetu kuwa zitaondoa yale malalamiko sugu yaliyoshindikana katika kipindi
cha takriban miaka hamsini sasa.
Mabadiliko
ya mfumo wa muundo wa Muungano ni suala lisiloweza kuepukika,hatuwezi
kukwepa ukweli wa udhaifu wa muundo wetu tulionao,tunahitaji mfumo
madhubuti,tusiogope mabadiliko ni hali ya mwanadamu kupitia vipindi
tofauti katika maisha.
Wimbi la
Serikali tatu kwa sasa ni kubwa unahitaji kuwa na chombo imara kwani
wimbi hilo la tufani linalotishia kulivunja Jahazi la mhafidhina ambapo
kwa sasa mabaharia wake wameanza kuweweseka baada ya jitihada nyingi
za kuwakatisha tamaa wataka mageuzi kutozaa matunda
Vuguvugu
la kutaka mabadiliko kwa kuwa na mfumo wa muundo wa Muungano wa Serikali
tatu siyo tu kwa Zanzibar bali ni Tanzania halikamatiki tena, hakuna
njia mbadala wala hekima inayoweza kuwatuliza wananchi zaidi ya
kukubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Jaji Warioba
kupendekeza Serikali tatu katika Muungano wetu.
Kizazi
cha leo na hata cha baadae cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kitaendelea kuwaheshimu wazee makini wa aina ya Jaji Marki Bomani ambao
hawakutaka kujizonga,hawakutaka kuficha uchafu kwenye zuria.
Mwanasheria
Bomani ataingia kwenye kumbukumbu ya watu waliosimama imara katika
kutetea mfumo wa muundo wa Serikali tatu,lakini hakusita kueleza hisia
zake kwamba hafungiki na wazo moja,ikiwa wananchi watataka mfumo fulani
hakuna budi kukubali matakwa yao.Alisema serikali tatu zitatoa nafasi
kwa kila nchi mwanachama kuendesha mambo yake jinsi wananchi wake
wanavyotaka.Jaji Bomani alisema ni vigumu kuunda mfumo wa muundo wa
Muungano ambao utamfanya mdogo kuwa na hofu.
“Kwa
kuondoa shaka hiyo, tuwe na Serikali tatu, ya Zanzibar,ya Tanganyika
zote zikiwa na madaraka kamili na kwa kuwa sisi ni wamoja lazima tuwe
na kitu kinachotuunganisha nacho
Aidha,
alishauri mjadala wa kupata katiba mpya uwe huru, wananchi wafungue
mioyo yao,wasifungwe na mawazo au itikadi fulani na badala yake kila
mmoja atoe alichonacho moyoni. CHANZO: MWANANCHI