Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, July 17, 2013

Huyu ndiyo mtu tajiri sana kuwahi kutokea duniani..Unajua alikuwa na utajiri wa kiasi gani?

us_20_21_pic_ rockefeller_john_d_1884
John Davison Rockefeller ndiyo mtu tajiri sana katika historia ya dunia hadi leo. Unaambiwa utajiri wake ukifananisha na hawa matajiri wa karne hii amewaacha mbali kupita kiasi. Ukichukua utajiri wa Bill Gates na Carlos Slim ambao wote kwa pamoja wana utajiri wa  billioni 140, lakini bado hata nusu ya utajiri aliowahi kuwa nao huyu jamaa bado hawajafikia. Mwaka 2007 mtandao wa Forbes ulirekebisha utajiri wa John Rockefeller baada ya inflation(mfumuko wa bei) na kukadiria kwamba alikuwa na utajiri wa dolla billion 663.4
John Rockefeller alifariki mwaka 1937 May 23 huko Florida akiwa na miaka 97, unaambiwa utajiri wake umetokana sana biashara ya mafuta ambayo kwa kipindi hicho ndiyo ilikuwa nishati mpya na inahitajika sana. Jamaa alianzisha kampuni inaitwa Standard Oil Company ambayo iliweza kufanikiwa kutawala soko la mafuta kwa kiasi kikubwa sana. Baada ya biashara kwenda vizuri akiwa na ndugu zake wa karibu, John Rockefeller aliweza kuwa mmarekani wa kwanza kufikisha utajiri wa dola billioni moja.
Zaidi ya biashara, John Rockerfeller alitumia utajiri wake mwingi kwenye ku-invest ndani ya masuala ya utafiti wa kisayansi kwenye mambo ya madawa ya binadamu,elimu na kusaidia watu kwenye foundation yake. Kwenye research alizowahi kuwekeza pesa zake na kuweza kupata mafanikio makubwa hasa kwenye kutokomeza janga la homa ya manjano kipindi hicho na minyoo inayoitwa hookworm.
Kumbukumbu ya John Rockefeller kwenye sekta ya elimu bado ipo hadi leo kwasababu yeye ndiyo muazilishi wa vyuo vikuu vitatu huko Marekani. University of Chicago, Rockerfeller Universityna Central Philippine University, vyote hivi vilianzishwa na John Rockerfeller.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...