
Rapper anaye
sifika kwa kuwa na maneno magumu kuelewa akiwa kwenye mahojiano na
watangazaji pale mjini Marekani, T.I Amefunguka kuhusu mtoto wake wa
kiume kuanza kufanya mziki aina ya rap na kusema kasha sikia wimbo alio
rekodi na ni mzuri kidogo, akitiwa madini zaidi ataweza kufanya vizuri
baadae.
Kuhusu
kolabo na Baba yake, T.I Amesema "Akiniomba kolabo nitamchana live kuwa
nina bei zangu za kushirikiana na wasanii na ili aweze kufanya kazi na
mimi lazima alipe kidogo, ila nitampunguzia malipo"
Mtoto wa
T.I Anaye rap anaitwa Domani na wakike anaye imba anaitwa Zonnique
anamiaka 14 na yupo kwenye kundi la R&B maarufu kama OMG Girlz
T.I
Amefafanua sababu za kumlipisha mtoto wake nakusema , lazima ajue ata
kama ni mtoto wa T.I,hio sio sababu yakupata vitu bure wakati wenzako
wanalipia.
Fahamu T.I Na familia yake wana kipindi kuhusu maisha yao kinachoitwa T.I & Tiny: The Family Hustle. Na kwa sasa T.I Yupo tour na Lil Wayne, French Montana na 2 Chainz.