Mbunge wa Arusha mjini Mh.Godbless Lema leo amefikishwa katika mahakama kuu kanda ya Arusha kwa kosa linalomkabili la kutoa maneno ya uchochezi kwa mkuu wa mkoa Arusha..


Tukio lililo tokea mnamo tarehe 24 mwezi wa Aprili katika chuo cha uhasibu Njiro ambapo wanafunzi hao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wakitaka kuonana mkuu wa mkoa pamoja na RPC ili kuzungumzia usalama chuoni hapo.

Akisomewa shitaka hilo mahakamani hapo ,wakili wa serikali Bi. Elianeny Njiro amesema mstakiwa Lema alifika chuoni hapo siku ya tukio na kuongea maneno kwa kutumia lugha ya uchochezi kwamba ‘amekuja kama anakwenda kwenye sendoff


Kauli hiyo ilichochea vurugu kwa wanafunzi kwa kupelekea wanafunzi hao kurusha mawe, chupa, wakati huo mkuu wa mkoa alipokuwa akitoa hotuba ,hali hiyo ilipelekea uvunjifu wa amani.


Aidha tukio hilo linatokana na mauaji ya mwanafunazi Henry Koga aliyefariki 23/4 kwa kuchomwa kisu na watu wasiofahamika na liliripotiwa polisi ambapo polisi waliweza kufika eneo la tukio na kufanya upelelezi ambapo upelezi huo uliendelea na mshtakiwa kufikishwa mahakamani .


Katika maelezo hayo wakili wa mshtakiwa bwana Method Kimomogoro alisema maelezo yanayokubalika na kwamba mshtakiwa tarehe 24/4/2013 alikuwepo chuoni hapo lakini maneno yaliyosalia kwamba alitoa maneno ya uchochezi sio ya kweli.

Hakimu aliyeendesha kesi Bi Devota Msofe alisema shauri la kesi hiyo litatajwa kwa siku tatu mfululizo ambazo ni tarehe 20,21,22 mwezi wa nane huku kukiwa na mashahidi kwa upande wa serikali ambao ni SSP Gilles Muloto wa polisi arusha, Inspecta Jane mkaguzi wa polisi arusha ,inspeta Benard nyambanya,PC Godfrey johachimu Wiliamu mahanyi wa polisi, Faraji kasidi wa chuo cha uhasibu njiro ,John Joseph wa chuo cha uhasibu njiro,Benjamini simkanga wa chuo, na naibu hamidu..


Hata hivyo mahakama iliridhia na shauri lililotajwa pamoja na mashahidi na dhamana kwa mshtakiwa inaendelea.