Baadhi ya watu wakiwa kwenye foleni ya kuingia katika uwanja wa ushirika kushuhudia Kili Music Tour.
Watu wakiwa wamelizunguka jukwaa la Kili Music Tour wakishuhudia show kutoka kwa wasanii mbali mambali wa hapa Tanzania.
Hapa Dj choka kushoto na Kassim a.k.a Babi D'e Conscious.
Nawapongeza sana waandaji wa mashindano ya Kilimanjaro
Tanzania Music Awards kwa jinsi ambavyo wamekua kichocheo kikubwa cha kukuza
mziki wa Tanzania na pia wamekua mfano mzuri wa kuigwa kwa jinsi ambavyo
wamekua wakiyaandaa mashindano hayo ambayo ni mashindano makubwa sana na yenye
heshima kubwa hapa nchini Tanzania.
Na kila mwaka mashindano haya hufanyika
jijini dar es salaam
lakini kwa kuwa waandaji wa mashindano haya wanatambua umuhimu mkubwa wa
washabiki na wapenzi wa muziki wa Tanzania waliopo mikoani wakaamua
kuandaa tamasha ambalo linafahamika kama Kili Music Awards Tour lengo
likiwa ni kuzunguka katika mikoa ya Tanzania ili mashabiki walioko
mikoani
nao wapate burudani kutoka kwa wasanii waliobahatika kupata tuzo na
husindikizwa na wasanii ambao pia kwa kipindi hicho wanakua wanafanya
vizuri
katika vyombo mbalimbali vya habari.
Kwa mwaka huu pia nazidi kuwapa pongezi
katika yale
wanayoendelea kuyafanya kwa kuwa kwa wao kuendelea kufanya hivi
wanavyofanya
naamini ni njia mojawapo ya kukuza mziki wa hapa Tanzania. Tamasha la
Kili Music Awards Tour liliyofanyia mjini
Moshi mkoani Kilimanjaro usiku wa tarehe 6/06/2013 kuamkia siku ya
tarehe
1/06/2013 naweza kusema ni tamasha ambalo limevunja rekodi ya kuwa na
watu wengi sana kwa hapa mjini Moshi na pia ni tamasha ambalo limekua na
mapungufu mengi sana.
Mazuri:
Tamasha hili lilifanyiwa matangazo ya kutosha katika vyombo
mbalimbali vya habari na katika mitandao ya kijamii. Matangazo hayo
yalifanikisha kwa kiasi kikubwa sana watu wengi sana kuweza kuhudhuria
katika tamasha la Kili Music Awards Tour ya mjini Moshi. Na iliweza kuwa na watu
zaidi ya elfu tano, wakiwemo watu wazima na watoto, wakazi wa mji wa Moshi na
wengine walitokea nje ya mji wa Moshi.
Walijitahia kuweka nyama choma na beer
aina ya Kilimanjaro za kutosha, pia waliweka viywaji aina ya grand malt
na maji kwa wale wasiotumia kilevi. Jukwaa pia
liliandaliwa vizuri sana
kwa ajili ya wasanii kuweza kufanya show na kila mtu aliyeweza kuingia
uwanja wa ushirika aliweza kuona kilichokua kikiendelea
pale jukwaani.
Nawapongeza sana
wasanii wa kundi la Jambo Squad (mamong’oo)
kwa kuweza kutoa burudani kwa mashabiki waliofika katika uwanja wa ushirika.
Wasanii wengine waliofanya vizuri ni Lady Jaydee (teamANACONDA), Roma
Makatoliki, Joh Makini, Kala Jeremiah, Diamond na Snura.
Mapungufu:
Watu walikuwa wengi kiasi ambacho tiketi ziliisha na
hakukuwa na njia mbadala ya kuweza kuwapatia watu tiketi zaidi ya watu kuwapa
walinzi wa mlangoni pesa na kuingia ndani kitu ambacho kilifanya waandaaji wa
tamasha hilo
kuzikosa pesa zile zilizoingia kwenye mifuko ya walinzi wa getini.
Waliruhusu watoto wenye umri wa chini ya
miaka kumi na nane kuingia uwanjani na matokeo yake liliibuka wimbi
kubwa sana la watoto waliopotezana na ndugu zao na katikati ya show
kulikua na matangazo ya kutangaza watoto waliopotezana na wazazi wao,
jambo ambalo halikua sahihi hata kitogo.
Waliofunga muziki/speaker hawakua wamejiandaa vya kutosha
kwa kuwa speaker zilikua zikikoroma na wakati mwingine zilitoa sauti kali
zilizokua zikiumiza masikio. Na wasanii walipokua wakiimba kulikua na tatizo la
muziki kuzima mara unarudi tena mara unazima na ilipelekea wasanii wengine
kushindwa kufanya vizuri jukwaani.
Poleni sana wasanii wa mjini
Moshi kwa kukosa nafasi hata moja ya kuonyesha vipaji vyenu kwenye tamasha kubwa
kama hili. Sio kawaida sana kuona tamasha lolote likifanyika mahali
popote bila kuwa na wasanii wachanga (undergrounds) wa mji au mkoa husika kupanda
jukwaani kuonyesha uwezo wao.
Wasanii walioshindwa kufanya vizuri jukwaani ni Barnaba Boy
yeye alishindwa kuwasiliana na Dj wake na mashabiki wake pia alionekana kutokuwa
na pumzi na pia kutokujiamini kwa kile alichokua anakifanya jukwaani.
Ben Paul yeye alionekana kujiamini katika kuimba lakini
hakuweza kuwasiliana na Dj wake na ilimfanya wakati mwingine kuimba na kufikia
katikati ya nyimbo na kuanza tena kuimba pia hakuwa amejiandaa na kufanya
mazoezi ya kutosha. Japo baadhi ya nyimbo zake zilionekana kuimbwa na mashabiki
wakati akiwa jukwaani lakini Ben Paul aliyekua jukwaani sio sawa na yule Ben
Paul aliyezoeleka kusikika kwenye radio na kuonekana kwenye TV.
Professor Jay: alionekana kuwa na mzuka sana lakini kwa
kweli kiwango chake kimeshuka na anahitaji mazoezi sana ili kuweza kuwa na
pumzi ya kutosha maana tayari ni msanii mkubwa na ni msanii ambaye amekua
kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa muda mrefu sana na watu wengi
walitegemea kuona vitu vipya na vyenye ubunifu wa hali ya juu ili kuweza
kuwadhihirishia watu kuwa yeye ni mkongwe na muziki anauweza. Sikutegemea
msanii mkubwa kama professor Jay angeweza
kupanda jukwaani alafu katikati ya show anaanza kumuita DJ Choka aje kufanyia back voco.
Vyoo navyo havikuwa vimeandaliwa kwaajili ya tamasha kubwa kama hili maana kwa mtu aliyeingia kwenye vyoo vya uwanja
wa ushirika vilikua vimejaa mkojo hadi ulikua ukimwagika nje kwenye jukwaa
ambalo watu walikua wamekaa.
Ushauri:
Wakati mwingine kukitokea tamasha kubwa kama
hili ni vyema waandaaji wafanye utaratibu wa kuuza tiketi sehemu tofauti na
pale getini na ikiwezekana waanze kuuza tiketi siku moja kabla ya tamasha au
siku hiyo ya tamasha tiketi zianze kuuzwa asubui na mapema. Na kusiwe na
utaratibu wa kuuzia tiketi mlangoni maana mara nyingi husababisha
msongamano/foleni kubwa sana.
Ni vyema wakati mwingine mkatafuta watu wa uhakika wenye
uzoefu mkubwa katika kuandaa matamasha makubwa ili kuweza kufahamu zaidi maana tunaamini
unapokosea jambo ndio mwanzo wa kujifunza na pia kuongeza ufanisi zaidi.
Waliopata nafasi ya kuchoma nyama pia walishindwa kufahamu
wakati gani ulikua wakati sahihi wa kuchoma nyama maana nyama ilikua ni ya
kuunga foleni na wakati tamasha linamalizika wachoma nyama ndio kwanza wanaweka
nyama na kuku kwenye jiko wakati watu ndio wanaondoka. Watu wengine waliondoka
na njaa kwa kuwa nyama ilikua ya kusubiria muda mrefu.
Credit: Kilimanjaro Blog