Jana nilikuwa mkoani Tabora nilikoenda kumsalimia kamanda Kileo na watuhumiwa wenzake wanaoshtakiwa kwa makosa ya ugaidi ya kummwagia tindikali Musa Tesha kipindi cha uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.
Lakini baada ya kuingia na kuonana na kamanda kileo nilipata mshtuko baada ya yeye kuniambia kuwa amezuiliwa kuvaa magwanda ambayo wanapenda kuyatumia CHADEMA na kutakiwa kuvaa nguo za kawaida.
Kileo alienda mbali zaidi pale aliposema kuwa hata nguo alizompelekea mke wake ambazo zilikuwa ni magwanda viongozi wa prison walizichukua na kumwambia kuwa atazivaa siku ya kwenda mahakamani,
Pia nikajaribu kufuatilia kuwa limeishia wapi ndipo nikapewa taarifa kuwa kuna mwanasheria mmoja(jina linahifadhiwa) toka hapa mkoani-Tabora alilifutilia suala hilo na kuambiwa kuwa viongozi wa magereza ya Uyui walipewa maelekezo toka kwa viongozi wa juu.
Pia akasema kuwa serikali inafanya hivo ili kupunguza nguvu ya CHADEMA ndani ya magereza kwani watu huishabikia sana.
Mungu tulinde na uipe mahakama nguvu
Source:Jamii forums