Naibu
waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu mwenye suti akipewa
maelezo na afisa wa maliasili juu ya gari lililotengenezwa kwa miti
ambalo linawavutia wengi bandani hapo Simba kivutio cha banda (PICHA NA TULIZO KILAGA WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
…………………………………………………………….
…………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
GARI ya
mbao iliyobuniwa na mkazi wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa, Keneth
Mwangoka imeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha
kuhifadhi mazingira katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.
Akizungumza
na MAELEZO katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba jijini Dar es
Salaam jana, Afisa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Msitu
wa Sao Hill mkoani Iringa, Fidelis Mwanalikungu alisema gari hiyo
ilibuniwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Sanaa cha Imehe kilichopo
katika kijiji cha Nyololo.
Alisema
kikundi hicho kwa kutumia gari hiyo ambayo huvutia watu kuiangalia,
kinaeleimisha vijini 58 vinavyozunguka msitu wa Sao Hill kudhibiti
matumizi ya moto unawashwa na wakulima wakati wa kuandaa mashamba yao
kwa ajili ya kilimo.
Alifafanua
kuwa uhamasishaji huo umefanikiwa kupunguza moto kutoka matukio 143
yaliyokuwa yanasababisha hekta za misitu 500 hadi 1000 kwa mwaka hadi
kufikia matukiio manne tu kwa mwaka yaliyounguza hekta 17 za misitu.
“Ukiweka
hizo hekta 500 hadi 1,000 katika thamani ya fedha unakuta tulikuwa
tunapoteza kuanzia Milioni 840 mpaka Bilioni moja kwa mwaka kutokana na
kuungua kwa msitiu huo, sasa hii ni hasara kubwa” alisema Mwanalikungu.
Alisema
kutokana na elimu inayotolewa kushirikisha kikundi hicho, wameweza
kuhifadhi zingira ya msitu huo wa asili wa Serikali, vyanzo vya maji na
kuhifadhi mazingira ya vijiji hivyo.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 uliobaini kuwa kutoka
mwaka 2010 kurudi nyuma miaka 11 kulikuwa kuna matukio mengi ya moto
yenye wastani wa matukio 143 kwa mwaka.
“Ilipofika
mwaka 2011 tukaangalia ni mikakati gani tunaweza kuichukua kwa
kuwashirikisha wanavijiji, ndipo tukagundua wazo la kusema tukiwa na
gari kama hili linalovutia watu, tukaweka mabango ya kuelimisha tunaweza
kufikisha ujumbe kwa urahisi zaidi” alisema Mwanalikungu.
Akizungumzia gari hiyo, Keneth Mwangoka gari hiyo aina ya Toyota Hiace aliinunua
kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma chakavu na
aliitengeneza ili iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata
njia ya kuwapata kwa urahisia wanakijiji a kufikisha ujumbe.
Mwangoka
ambaye ni fundi wa gari hiyo, alisema gari hiyo ina injini ya Toyota
1S, robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta lita
moja kwa kilomita nane.