Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) ambaye pia ni Malikia wa Taji la Mkoa wa Morogoro Diana Laizer (21) ( katikati) akiwa na wenzake mshindi wa pili , Sabra Islam (19) ( Kushoto) pia kutoka Mkoa wa Morogoro pamoja na mshindi wa tatu Janeth Awet ( 19) kutokaMkoa wa Lindi mara baada ya kutagazwa washindi katika shindano lao lililofanyika Juni 29, mwaka huu.
Madensa wa Kundi la Msanii wa kizazi kipya Tundaman, wakishambulia jukwaa.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, wakiwa katika vazi la jioni.
MC katika shindano la kumpata malkia wa Taji la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Kaka Aidan Ricco ambaye ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania akielezea utaratibu wa kuwapata washindi watano.
Mshiriki Zulfa Semboja kutoka mkoa wa Mtwara akionesha vazi la ubunifu mbele ya watazamaji
Washindi wanne wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 wakisubiri Jaji Mkuu kutaja majina yao katika nafasi ya ushindi kuanzia kwanza, pili , tatu na ya nne.
Mwanamuziki wa Kike wa kizazi kipya, Keisha ( wa kwanza kulia) akipiga makofi kufurahiamchuano wa warembo wa Redd's Miss Kanda Mashariki , Juni 29, mwaka huu
Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 yenye taji kishwani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wenzake waliokuwa wameingia tano bora.
Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Diana Laizer akifurahia kitita cha fedha alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa
MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka
Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM), Diana Laizer (21) amefanikiwa
kunyakua taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki baada ya kuwashinda
wenzake 12 walioshiriki kuwani taji hilo mwaka 2013.
Mshindi
huyo ambaye pia ni malkia wa taji la Redd’s Miss Morogoro 2013 akiwa
amevalia namba sita ya ushiriki ,amefanikiwa kuchukua mikoba ya
mtangulizi wake Rose walifanikiwa kunyakua taji hilo juzi usiku katika
ukimbi wa Nashera Hoteli wa Mjini hapa baada ya kutangazwa na majaji wa
shindano hilo.
Jaji
Mkuu , Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, mbali
na kumtangaza malkia wa Kanda ya Mashariki , alimtangaza pia mshiriki
kutoka mkoa wa Morogoro Sabra Islam (19) kushika nafasi ya pili katika
kinyang’anyiro hicho.
Sabra aliingia kwenye shindano
hilo baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano ya Redd’s Miss
Morogoro 2013 ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe. Kwa mujibu
wa Jaji Mkuu huyo, mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kanda ya Mashairiki
ilitwaliwa na mrembo Janeth Awet ( 19) kutoka Mkoa wa Lindi na nafasi ya
nne ilinyakuliwa na mrembo Elizabeth Perty (22) kutoka Mkoa wa Pwani.
Makoye alisema kutokana na washiriki wa kinyang’anyiro hizo Kanda ya
Mshariki kuwa na warembo karibu wote wenye sifa na vigezo.
Kamati
ya Miss Tanzania imeamua kuwachukua washiriki wanne kuingia katika
kambi ya shindano ya Miss Tanzania mwaka huu. Hata hivyo alimtaja
mwingine aliyeingia tano bora ni Ivon Stephen (22) kutoka Mkoa wa Mtwara
, ambapo wengi walioshiriki na mikoa yao katika mabano ni Zulfa Semboja
(19) ( Mtwara) na Pulkeriah Ndovi (21) ( Mtwara).
Wengine
ni Sophia Maganga (21), Lindi, Zainabu Shaaban (23) (Lindi), Lilian
Joseph (21) ,(Pwani ) Easther Albert (20) ( Pwani), Muzne Abduly ( 19)
na Ummy Mohamed (21) wote ni kutoka Mkoa wa Morogoro. Naye Mratibu wa
Shindano hilo, Alex Nikitas, aliwakabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza
sh: 600,000, Mshindi wa pili sh: 400,000 na mshindi wa tatu sh: 300,000 ,
ambapo mshindi wanne na watano walipatiwa sh: 200,000 kila mmoja na
wengine waliobakia kusawadiwa sh: 100,000 kila moja.
Katika
shindano hilo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa ,
Mustafa Mkulo na pia kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo na Mbunge wa
Jimbo la Gairo , Ahmed Sabiby pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,
Jaji Frederick Werema ambapo pia mwanamuziki wa kizazi kipya Tunda Man
walitumbuiza likiwemo na kundi la sanaa la Wanne Star.