Julai 5 2013, Dar es Salaam
Chemba
ya Madini na Nishati Tanzania, inaipongeza serikali kwa kuanzisha Mradi wa Matokeo
Makubwa Sasa. Baada ya kushuhudia uzinduzi wa miradi ya kitaifa katika sekta ya
nishati uliofanywa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo,
uzinduzi uliofanyika Mlimani City tarehe 3 Julai, 2013, Katibu Mtendaji wa TCME
alisema, “wajumbe wetu katika tasnia ya madini wanafuatilia kwa makini
maendeleo katika sekta ya nishati kwa sababu ya mabadiliko yatakayosababisha
kwenye maendeleo ya sekta ya madini. Tunaipongeza Wizara ya Nishati na Madini
kwa jitihada na ahadi hizi za utekelezaji.”
Makampuni ya uchimbaji madini
Tanzania ni mojawapo ya watumiaji wakuu wa nishati nchini, lakini mara nyingi
yanahitajika kutengeneza nishati yake kwa kutumia mashine makubwa na ghali ya
kutumia mafuta. Upanuzi wa gridi ya taifa kuelekea Kaskazini Magharibi mwa
Tanzania kutafanya uchimbaji madini kuwa uwekezaji wa kuvutia zaidi. Masuala
mengine yote yakiwa sawia, migodi iendeshwayo kwa nishati ya uhakika ya gridi
ya taifa inapunguza gharama kwa wazalishaji na kuwawezesha kujenga migodi zaidi
na kupanua miundombinu ambayo tayari wanayo, na hii inapelekea utengenezaji wa
ajira na inaongeza malipo ya kodi kwa serikali.
“Matokeo Makubwa Sasa ni hatua
ya bashasha sana” Bwana Jengo alisema, “ Tuna uhakika kuwa kwa pamoja, wenzetu
serikalini na wale wa sekta binafsi tutafanikisha manufaa ya moja kwa moja na
yanayoshikika kwa Tanzania na jamii yetu ya kibiashara. Inawezekana endapo kila
mmoja wetu atatekeleza katika nafasi yake.
“Mradi wa Matokeo Makubwa Sasa
hauishii kwenye umeme. Makampuni ya uchimbaji madini na nishati yanafurahishwa
na maboresho ya miundombinu. Bandari bora zaidi, barabara zilizoboreshwa na
reli zilizowekwa katika hali nzuri zitasaidia kuongeza ari ya uwekezaji katika
nchi yetu. Imani kwa miradi mingi ya ndani ambayo wanachama wetu wanazifanyia
kazi itaongezeka tu kwa uwepo wa usafiri wa kisasa na uboreshaji wa uwezekano
wa maendeleo.”