Na John Banda, Dodoma
WAKAZI
 wa Manguruweni  kata ya Tambukareli manispaa ya Dodoma wameishutumu 
mamlaka ya Ustawishaji makao makuu CDA kutokana na Kuwabomolea  nyumba 
yao wakati shauri lipo mahakamani.
Wakazi hao waliokutwa na mwandishi wetu wakiwa hawana la kufanya baada ya nyumba iliyopo eneo hilo kubomolewa na maaofisa wa CDA waliokuwa na ulinzi mkali wa polisi na vifaa vya ndani vikiwa vimezagaa  nje ya moja ya nyumba hizo zilizobomolewa pamoja na watoto wao huku nyumba hiyo ikiwa imebomolewa upande wote  wa nyuma na kuachwa kwa mbele.
 Mwenye
 Nyumba hiyo Alfonce Kishe Alilipasha Jambo leo kuwa  msafara wa jumla 
ya magali sita  yakiwemo ya polisi mawili na katapila la kubomolea 
yalitinga katika nyumba hiyo majira ya saa nne asubuhi akashanga kuona 
asikari wenye aina mbalimbali za silaha wakaizingira
nyumba yake.
Kishe
 alisema baada ya kuona vile akawauliza maafsa wa CDA ambao aliwatambua 
kutokana na Sale walizokuwa wamevalia na magali waliyokuja nayo, vipi 
mbona walimvamia bila taarifa yoyote na kuambiwa ni 
yeye aliyewasababisha wafike kuvunja kutokana na wao kwenda mahakamani.
‘’Ndugu
 yangu nilipowauliza kwanini waliniambia eti wanavunja kwa sababu sisi 
tulienda mahakamani  kuwashitaki kwa wao kutaka kutuondoa katika aridhi 
yetu tuliyoachiwa na marehemu baba yetu na nyumba hii tuliijenga 1993 
pamoja na hii miti 19 unayoiona hapa na miwili wameivunja hivi hii ni 
haki kweli CDA hawajili hata mahakama wakati jana tumekuwa baraza la 
aridhi na tumepangiwa tarehe 30 mwezi huu’’, alihoji Kishe
Aidha
 Kishe aliongeza kuwa mwaka jana ndipo walipoanza kusumbuliwa na watu 
mbalimbali alioita wanalimezea mate eneo lao hilo lenye ukubwa wa 1/4 
robo tatu heka lililopo nyuma kidogo ya chuo cha Biashara CBE, na mwezi 
mei mwaka huu wakapelekewa  Barua ya kutakiwa kubomoa na kuondoka ya 
siku 14, na wao kuamua kwenda Baraza la Aridhi.
Alisema
 Baada ya kwenda baraza la Aridhi wakapangiwa tarehe 10 julai 2013 
kusikilizwa na baada ya kusikilizwa kesho yake wakavunjiwa huku wakiwa 
hawajui ni wapi pa kwenda kulalamikia wala kusaidiwa baada ya kuachwa 
nje pamaja na familia zao wasijue watakapolala wala kujificha jua.
Kaimu
 Mkurugenzi wa CDA Mtemi John alikanusha kuwa eneo hilo si la huyo 
mlalamikaji na kwamba tayali mwenye eneo hilo alishapewa kiwanja kingine
 mbadala na wao hawawezi kuvunja eneo lolote kinyume na Sheria na kwamba
 kila mtu anayetaka kufanya lolote katika aridhi inayomilikiwa na 
mamlaka hiyo lazima awe na kibali.
 Alisema
 tayali alishapewa mtu mwingine tangu mwaka 2002, na  2003 ndipo huyo 
mlalamikaji akavamia na kujenga na hata hivyo kwa busara walishampa 
kiwanja mbadala na 32/2 na hata hivyo mmiliki wa pili  kuwa hawezi 
kufanya kazi kwa kusikiliza maneno ya mtaani na kama watafanya hivyo 
kuweka mpangilio wa mji vizuri utashindikana.
‘’Unapotaka
 kujenga mji uliopangika lazima ukabiliane na malala miko ya watu  kwa 
sababu unagusa masrahi ya yao,  hatuwezi kuacha tunakaza uzi mpaka mji 
wa Dodoma ukae kimpangilio kama ilivyo sasa ni zaidi ya asilimia 70 kuwa
 umepangika kinyume na mikoa karibu yote nchi’’, alisema Mtemi 
 
 





 
 
 
