WAZIRI
Mkuu David Cameron na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza wamekuwa
miongoni mwa watu mashuhuri waliotoa pongezi kwa mchezaji tenisi nyota
wan chi hiyo Andy Murray kwa kunyakuwa taji la michuano ya
Wimbledon. Wachezaji nyota na watu wengine maarufu nchini humo pia
walitoa pongezi zao kwa Murray mwenye umri wa miaka 26 baada ya kuwa
Muingereza wa kwanza kunyakuw ataji la michuano hiyo toka Fred Perry
alipofanya hivyo mwaka 1936, kwa kumfunga Novak Djokovic kwa seti 3-0.
Cameron
ambaye alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo alimpongeza Murray
kwa kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo na kuweka historia mpya
katika mchezo huo nchini Uingereza. Mwandishi wa BBC katika kasri ya
kifalme nchini humo, Peter Hunt alibainisha kuwa Malkia alimtumia ujumbe
binafsi Murray kumpongeza kwa kufanikiwa kushinda taji hilo.