siku hizi
camera za simu ndio kila kitu watu wameacha kununua digital camera za
kawaida na watu wanatumia camera za simu kila wakati. ni vigumu kujua
uzuri wa camera ya simu hadi upate maelekezo kidogo. hapa nimejaribu
kuchambua simu zenye camera bora zaidi duniani na nimezigawanya katika
makundi matatu 1. kundi la kwanza- simu zilizotoka muda mrefu nimezigawanya
kama simu zilizotoka muda mrefu sababu simu hizi sasa hv zimeshuka bei,
unaweza ukazipata mkononi kwa bei rahisi na zinapatikana maeneo mengi,
hapa tunapata cameraphone 2. NOKIA 808 pureview nokia 808 ndio
simu ya kwanza duniani kuwa na camera yenye lens ya 41 megapixel, hadi
leo inaaaminika ndio camera phone bora duniani. simu hii inatumia
symbian specification zake sio za kutisha sana na ina processor mbili
moja ya simu na nyengine kwa ajili ya camera tu. nokia 808 ina camera
yenye akili ambayo unaweza kubadilisha vitu vingi vya profesional
photographer kama iso, white balance na vyenginevyo. silaha kubwa ya
hii camera ya simu au unaweza kuita engineering trick inaitwa pixel
oversampling. yani hii nokia 808 ina megapixel 41 lakini inatoa picha
hadi za megapixel tano, inachofanya inapiga picha nyingi (kama 7) halafu
inaunganisha zile picha kwa kushibisha pixel (pixel 7 zinaunganishwa
kutoa super pixel yenye quality nzuri) hii inafanya picha za hii simu
kuwa zina quality kubwa sana. watu
wanaotakiwa kumiliki simu hii ni wale wanaopenda camera nzuri kwa bei
rahisi, wanaopenda symbian, wasiojali kuzoom sana, wanaopenda quality ya
picha za kushare kwenye social site kama facebook, instagram. bei yake
kwa sasa unaweza pata rahisi hadi 600,000 GALAXY CAMERA hii ilikua ni
karata ya kwanza ya samsung kwenye soko la camera phone. simu hii
inatumia android na ina specification kubwa kushinda nokia 808. galaxy
camera yenyewe ina lens ya 16 megapixel. simu hii haitoi picha zenye
quality kubwa kama 808 na haina akili kama 808 lakini ina silaha yake
yakipekee ambayo 808 haifikii nayo ni zoom. ina lens ambayo inazoom kitu
kilicho mbali kije karibu hii simu ni
nzuri kwa waandishi wa habari, na watu wanaopenda kupiga picha kutokea
mbali bei ni around 800,000 kama unaweza kutoa hela zaidi ya hiyo na
umeipenda aina hii ya camera ya simu ni vizuri ukaenda kununua galaxy s4
zoom ambayo ntaielezea hapo chini. 2.kundi la pili simu zilizotoka sasa hapa sasa
hakuna kulia lia bei hizi ni brandnew camera phone ambazo zimetoka siku
si nyingi ndio nzuri zaidi kimuonekano na pia zinakuja na latest
features za smartphone. LUMIA 1020 imetoka juzi
july 11 mwaka huu ikiwashangaza wengi sana baada ya nokia kuweza
kuunganisha technolojia zake mbili za pureview za mwanga mdogo na pixel
oversampling ina maana hapa unapata uwezo wa camera ya lumia 920 na
nokia 808 pureview kwenye camera moja. ni nyembamba imeekwa kifashion
zaidi pengine hii ndo camera ya simu ianyovutia zaidi masista duu,
mabitozi, mnaopenda fb na social network, wandishi wa habari na wapenda
camera wooote hiii ndio camera phone bora zaidi kwa sasa. bei ni around
1,300,000. imeanza kuuzwa marekani sasa mwez wa 9 itasambaa duniani. GALAXY S4 ZOOM wote tunaijua
samsung galaxy s4, flagship ya samsung sasa hii ni version yake ya
camera. usitegemee specs za s4 humu hii imepitwa specification na hata
galaxy camera lakini ndio latest camera phone ya samsung. kama alivo
mdogo wake silaha kubwa ya hii camera ni zooming ikiwa na lens kubwa
kabisa kama hujali
specs sana unaweza ku upgrade toka galaxy camera kuja huku maana camera
hii ni nzuri zaidi. watu wanaotakiwa kununua ni wale wale kama wa galaxy
camera na bei ni around 900,000 au 1m 3. kundi la tatu ni kamera tunayoisubiria galaxy camera
zimeshindwa kuonesha ubavu kwa nokia lakini yupo ambaye watu
wanamsubiria kuja kumpa upinzani nokia ambaye si mwengine bali ni sony
honami. hii simu itatoka muda si mrefu na itakua na megapixel 20.