Mgombea
Udiwani katika Kata ya Elerai kwa tiketi ya CHADEMA, Jeremiah Mpinga
akielezea namna Mwigulu Nchemba, CCM, alivyofika nyumbani kwake na
kumtaka aachane na siasa za CHADEMA.
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa katika uchaguzi
mdogo unaotarajiwa kufanyika Julai 14, 2013, kitahakikisha kitatumia
gharama yoyote kuzilinda kura katika Kata nne jijini Arusha.
Akiongea
na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho Mkoa, maarufu kwa
jina la “Ngome”, Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alisema
kuwa uchaguzi wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Jumapili katika Kata za
Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai utakuwa wa aina yake.
Mhe. Lema
alisema kinyang’anyiro hicho cha Kiti cha udiwani kitasimamiwa na vikosi
maalum vya chama hicho sanjari na vijana wao wa “Red Brigade” huku
Wabunge zaidi ya 16 wakitarajiwa kuwasili Arusha kwa ajili ya
kuhakikisha ulinzi wa kura unaimarika.
“Ulinzi
wa kura zetu umeimarika kwa asilimia kubwa na tutashinda Kata zote kwani
hadi sasa tunazo asilimia 80% ya ushindi,”alisema Lema.
Naye
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha, Joshua Nassari
amelalamikia kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi katika
mapokezi yake huku wakigomea kufanyika kwa mkutano wa hadhara jimboni
kwake kwa madai kuwa utavuruga uchaguzi.
Mhe.
Nassari aliyasema hayo muda mchache mara baada ya kuwasili Mkoani Arusha
ambapo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili huku akiweka wazi
kuwa anaendelea vizuri na yupo gado kwa mapambano
“Nimefika
airpot Dar hali ni tete baada ya kuona polisi kila kona, hapa Arusha
hivyo hivyo huku wakiwa na magari zaidi ya 6… Kwa nini wasilinde
rasilimali za nchi? Kama tembo wanaoibiwa kila siku waje wahangaike na
mimi ambaye naenda kuongea na wananchi wangu,” alihoji Nassari.
Naye
mgombea udiwani wa Kata ya Elerai, Mhandisi Jeremia Mpinga amekanusha
vikali tuhuma za kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha udiwani wa Kata
yake kama ilivyotangazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii.
Mpinga
likwenda mbali kwa kusema kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba
alifika nyumbani kwake na kumtaka aache kugombea kwa tiketi ya CHADEMA
na kumwahaidi kuwa atapewa Ukuu wa Wilaya na Mhe. Rais Jakaya Kikwete.
“Alinipigia
Jun1 12 majira ya saa tatu asubuhi akitaka kuja kwangu kuniona, akaja,
na ndipo aliponipa ujumbe huo wa ukuu wa Wilaya,” alisema Mpinga.
picha, maelezo via Jamii Blog