Mwigizaji
wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema yeye
na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki historia na kamwe
hawawezi kurudiana naye japo anayajua mapenzi.
Akizungumza
na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema ameshaamua
kujituliza kwa mpenzi wake wa sasa hivyo hata iweje hawezi kurudiana
na Bond.
Jamani
kwa sasa mnaona nimebadili kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond
atabaki kuwa rafiki kama walivyo marafiki zangu wengine.
“Niliwahi
kuachana naye kipindi flani baadaye tukarudiana kutokana na ukweli
kwamba ni mwanaume anayejua kupenda na anayajua mapenzi ,lakini
hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu.