Mtandao wa
bongo movies umetumiwa madai, kumhusu mwanadada muigizaji wa Filamu
aliyepata tuzo hivi karibuni, Jennifer Kyaka anakwenda na jina la
kisanii la Odama kuhusu safari zake za kwenda nje ya nchi. Habari
au tuhuma hizi , zinasema kuwa mwanadada huyo huwa haendi nje ya nchi
kama anavyowaambia washabiki wake kupitia blog yake ya
odama1.blogspot.com kuwa anasafiri kwenda nje kikazi zaidi, na badala
yake imesemwa kuwa huwa anabaki hapa hapa nchini akijifanya yupo nje ya
nchi,akiwa na lengo la kutafuta kulazimisha umaarufu
ushahidi wa picha mbalimbali toka kwenye mtandao mmoja wa kijamii
ambao staa huyo Mdau aliyepeleka tuhuma hizo, amesema kuwa ana ushahidi
wa kutosha na katuma anautumia kudanganya zikimuonesha akiwa maeneo
mbalimbali ya “duniani huko” ambayo kwa kuangalia picha hizo anasema
kuwa ni feki na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia tu ya kuhariri
picha maarufu kama“PHOTOSHOP”Mtandao
wa Bongo Movies umewaomba wadau wenye majibu na utaalamu wa picha
wasaidie kwa kutazama picha hizi ili kuthibitisha kama tuhuma hii ina
ukweli wowote.