HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina
Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’
wanadaiwa kumwagana rasmi
Habari kutoka chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa wapenzi hao, zilieleza kuwa Amanda na Bwana Misosi walishamwagana kimyakimya ikiwa ni baada ya kushindwa kuelewana kitabia.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.
“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza kujuta,” alisema Amanda.
Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
“Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi.