Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI
la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali
Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika
manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa
mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa
na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo
limehifadhiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu
kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo
la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea
hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo
tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo
vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.
Chiposi alisema kuwa
wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito
walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya
kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa
nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye
alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.
Alifafanua zaidi
kuwa wazazi wa msichana huyo ambao hakutaka kuwataja majina yao
walifanya upelelezi wa kina ambao uliwalidhisa kuwa tukio hilo
limefanywa na mfanya biashara huyo ambaye alikuwa amekaribishwa kuishi
kwenye nyumba yao baada ya kutengana na mke wake wakati akisubiri
kugawana mali walizochuma kwa pamoja.
Alieleza zaidi kuwa
mtuhumiwa Nassoro kwa hivi sasa anashikiliwa na polisi lakini yupo
hospitali ya serikali ya Mkoa Songea(HOMSO) ambako amelazwa akidai kuwa
anasumbuliwa na BP ya kushuka na kwamba Jumatatu ijayo anatarajiwa
kufikishwa mahakamani na hata kama atakuwa hajaruhusiwa atasomewa
mashtaka yake yanayomakabili akiwa amelala kitandani kwenye hospitali
hiyo kwani upelelezi wa tukio hilo umeshakamilika.
Kwa upande wake
mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) Dkt. Benedkto
Ngaiza amethibitisha kumpokea mfanyabiashara huyo Jamali Nassoro ambaye
alipelekwa hopitalini hapo akiwa chini ya ulinzi mkali na amelazwa wodi
ya wanaume namba saba akiwa anaendelea kupata matibabu. VIA/demashonews
|