Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (pichani) amesema iwapo Mfumo wa Serikali Tatu utaridhiwa na wananchi ni lazima mambo yaliyo ndani ya Muungano yatagawanywa ikiwa ni pamoja na Ikulu ya Rais.
Amesema
kuwa kutokana na taifa kufanya mabadiliko ya Katiba ni lazima kuwepo
mpangilio wa kugawana mambo mbalimbali yaliyokuwa chini ya Muungano
ikiwamo majengo, wafanyakazi, Ikulu, hata vitendea kazi na kwamba
utaratibu huo ni kama ule uliotumika wakati Tanganyika na Zanzibar
zilipoungana.
Kauli
ya hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku tatu tangu Waziri wa Katiba na
Sheria, Mathias Chikawe kueleza kuwa Tanzania Bara itaanza mchakato wa
kutunga Katiba yake Aprili mwaka 2014 na kumalizika Desemba mwaka
huohuo.
Jaji
Warioba aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na waandishi waandamizi
wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha
magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili,
Mwanaspoti, The Citizen na The Citizen on Sunday, Tido Mhando ambaye pia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL na Theophil Makunga, Meneja wa Uendeshaji
na Biashara MCL.
Warioba: Ukibadili Katiba wakati wowote ni lazima kuwe na makubaliano fulani.
Unajua
Serikali ya Muungano na Tanganyika ilikuwa pamoja, sasa ukianzisha
Serikali ya Tanganyika, lazima kwenye mpangilio muanze kugawana hata
wafanyakazi kwa kuwa wafanyakazi hao walikuwa ni wa Muungano. Hapo ndiyo
mtaamua wafanyakazi gani watakwenda katika Serikali ya Tanganyika,
watakaobaki katika Muungano na wale watakaokwenda Zanzibar.
Hata
katika majengo hali inakuwa hivyo hivyo, lazima kutakuwa na majengo
yaliyokuwa yakitumiwa na wizara mbalimbali na hata Ikulu. Hapo pia
lazima myagawanye na kukubaliana viongozi wa Tanganyika watakuwa wapi na
wale wa Muungano watakuwa wapi. Lakini, hata vifaa vya kutendea kazi
navyo inatakiwa mgawane kulingana na makubaliano yenu.
Suala
hili linategemea zaidi mazungumzo ya pande zote mbili, baada ya
kukamilika kwa mchakato huu kwa sababu hii iliyopatikana sasa ni rasimu
tu, ambayo itajadiliwa na wananchi kabla ya kuanza kwa Bunge la Katiba
na baadaye kuwepo kwa kura ya maoni. Wapo watakaokuwa wakihoji kuhusu
vyeo, katika hili itakuwa kama tulivyokuwa tukiungana Tanganyika na
Zanzibar, wakati huo wapo ambao walikuwa wakuu wa mikoa na wakajikuta
wameingia katika Muungano huku wakiwa na vyeo hivyo. Kilichofanyika ni
kuendelea tu na nafasi hizo mpaka utakapofanyika utaratibu mwingine kwa
njia ya mazungumzo.
Unajua jambo hili siyo jukumu la tume hii, tunaliacha kwa sasa na hatujui litakuwaje kwa sababu ni suala la mazungumzo.
Swali: Majukumu ya Rais yatakuwaje?
Warioba: Rasimu imeeleza majukumu (roles) ya Rais kama mkuu wa nchi, ambaye anakuwa kama taasisi na sisi tulichokifanya ni kujenga taasisi hizo, kwamba ijulikane akifanya chochote awe ameshauriwa, isiwe yeye peke yake.
MWANANCHI
Warioba: Rasimu imeeleza majukumu (roles) ya Rais kama mkuu wa nchi, ambaye anakuwa kama taasisi na sisi tulichokifanya ni kujenga taasisi hizo, kwamba ijulikane akifanya chochote awe ameshauriwa, isiwe yeye peke yake.
MWANANCHI