Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 10, 2013

WALIOSHIRIKI KUPINGA FREEMASON NA UASI WA LIONS CLUB NA ROTERY CLUB


  Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons



wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).
Mohammed Sayed Tantawi
Katika miaka ya 1970 kiongozi wa juu na Sheikh wa Chuo kikuu cha kiisilamu huko Misri (Egypt) inasemekana alitoa fatwa kuwakataza waisilamu wasijiunge na chama cha Rotary Club na wakati mambo haya yalikua yakikatazwa na dhehebu la sunni Chama cha rotary pia kilisikika kukatazwa na Ayatollah Khomeini.

Ayatollah Khomeini
katika mwaka wa 1798 Mwandishi Mmoja wa Kiingereza aliejulikana kwa jina la john Robbinson aliandika kitabu kijulikanacho kama Proofs of a Conspiracy Against All the Religions and Governments of Europe, Carried On in the Secret Meetings of Free Masons, Illuminati, and Reading Societies (Uthibitisho wa njama dhidi ya Dini zote na Serikali zote za Ulaya ilipangwa katika mikutano ya siri ya Freemasons, Illuminati, na vyama vinginevyo vya Reading)

John Robbinson
Kitabu hicho kinaelezea Ari na hamasa za Freemason walivyokuwa wakipanga kisiri jinsi ya kupinduwa mipangilio mizuri ya Maisha (Serikali) na ndio waliosababisha mapinduzi nchini Marekani na Ufaransa.

Shuku za kuenea kwa Freemasons zilienea hadi kufikia miaka ya 1800 ambapo
Rais Wa 13 Millard Fillmore wa Marekani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)

Sergiei Nilus Mwandishi Kitabu cha Protocol
Kitabu cha The Protocols of the Elders of Zion sio kuhusu mayahudi kutawala dunia lakini ni kuhusu njama za freemason wa kiyahudi kubadili mfumo wa dunia.

Hitler Reinhard Heydrich
Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.

Moqtada al-Sadr Al Hawza
Nchini Irak, Gazeti la Moqtada al-Sadr lijulikanalo kama Al Hawza lilichapisha picha ya George H.W. Bush na Bill Clinton na akaelezea kwamba ishara ya mikono yao ilikuwa ni alama ya waandamizi wa kizayoni na freemason, na kama walivyo Wakatoliki Waisilamu pia waliwahusisha wanchama wa Rotary moja kwa moja na Freemasons na kusema vyama vyote viwili ni laana.

Rais Bush Rais Clinton
Freemasons wamehusika moja kwa moja katika jitihada za kutawala Mashariki ya kati jitahada ambazo zilibuni uhasama kati ya Mashariki ya Kati na Jumuiya ya Magharibi.
Freemason walitoa fursa ya wafanyabiashara kuunda mtandao mmoja, hii ni katika malengo ya wafanyabiashara wanachama wa Freemason wa Ulaya wafungue ofisi za Freemason nje ya nchi na kuwaalika wanainchi wa Ulaya kujiunga nao.

Kwa ujumla sio Wafanya biashara wa Wakiingereza au Mashariki ya kati ndio waliowengi tu kama anavyoeleza bwana Hamid Algar wa Berkeley ambaye ni Mwanachuoni maarufu duniani wa historia ya Kiisilamu:-

Hamid Algar
Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...