NA SULEIMAN MSUYA
WAKATI
Dunia ikijianda kwa maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa seli ya damu
(sickle Cell) kesho kutwa Juni 19, Tanzania ina madaktari wa kutibu
ugonjwa huo wanne tu jambo ambalo linaweza kusababisha ongezeka kubwa
la wagonjwa.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Motion Arts Production (MAP),
Honeymoon Aljabri ambapo wanatarajia kufanya maonyesho ya michoro
inayoonesha rasilimali za nchi ya Tanzania pamoja na kujadiliana na
wadau mbalimbali juu ya ugonjwa huo.
Alisema
takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na
wagonjwa wengi wa Sickle Cell, hivyo ni wakati muafaka kwa kila mtu
kujitokeza kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo.
Aljabri
(MAP) inatarajia kufanya onyesho la sanaa ya uchoraji Juni 17 mwaka huu
katika Jumba la Makumbusho ya Taifa) ambapo onyesho hilo litawezesha
watu mbalimbali kujadiliana kuhusu Siko Seli wakati wanatembelea
michoro hiyo ambayo itakuwa inahusu rasilimali mbalimbali zilizopo hapa
nchini.
“Kesho
kutwa Jumatano ni siku ya Sickle Cell Duniani ila ni vema Watanzania
wakatambua kuwa nchi yao ina waathirika wengi kwani ni ya nne duniani na
ina madaktari wane ambao hawatoshi,” alisema.
Muasisi huyo wa MAP pamoja
na kutumia maonyesho hayo pia anatarajia kufanya matembezi ya kilometa
tano mwezi Septemba ambao ni mwezi uliopangwa duniani kote kuwa mwezi wa
kupata elimu kuhusu ugonjwa huu wa Siko Seli.
Aljabri
alisema katika matembezi hayo wanatarajia kuchangia damu pamoja na
shughuli nyingine mbalimbali za kijamii ili kuweza kuwasaidia waathirika
wa ugonjwa huo hapa nchini.
Mkurugenzi
huyo alisema mwaka huu wataendesha kampeni hiyo katika mkoa wa Dar es
Salaam pekee ila matarajio yao ni kuhakikisha kuwa kwa miaka ijayo
wanafika kwenye mikoa yote nchini.