Na Mahmoud Ahmad Arusha
Serekali imesema kuwa itafanya
kila jitihada kuhakikisha kuwa wale ambao wamehusika na tukio la
ulipuaji wa bomu uliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni wa
chadema watatiwa mbarano na kuchukuliwa
hatua kali za kisheria.
Hayo yamebainishwa na makamu wa
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal
wakati alipowatembelea wahanga wa bomu lililorushwa June 15 mwaka huu
katika mkutano wa chadema .
Alisema
kuwa serekali imepokea kwa masikitiko makubwa jambo hili ambalo ni la
kigaidi na hatasita kumchukulia mtu yeyote aliyehusika na tukio hili
hatua kali za kisheria iwapo atakamatwa .
Aliwataka wananchi wavute
subira,wawe wastamilivu na pia wavumilivu haswa katika kipindi hichi
ambacho upelelezi unaendelea na wasikate tamaa hata kama itachukuwa
muda mrefu.
“napenda
kuwaambia msikate tamaa vuteni subra kwani aliyehusika atakamatwa tu
hata kama ikitumia muda wa siku tatu ,siku kumi mwezi na hata miaka
mitatu na zaidi lakini aliyefanya tukio hili atakamatwa tu
ata akienda wapi nanachopenda
kuwaambia wananchi kuwa mjenge imani na serekali yanu ya jamuhuri ya
muungano wa tanzania na mshirikiane nao na mwishowe matatizo haya
yatakwisha”alisema Bilal
Aidha
aliwataka wananchi wajenge imani na mapenzi mema na makubwa kwa nchi
yao na hiyo tu ndo itawasaidia kuwavusha katika katika matatizo haya
ambayo yanatokea kwa kwa kipindi hichi huku akiwasisitiza kuwa iwapo
watajenga imani na mapenzi na serekali yao basi nchi yetu
itakuwa na amani kama zamani na historia yake itaendelea kubaki kuwa Tanzania ni nchi ya amani .
“pia napenda kuwaambia kuwa
tusikubali mtu atuvuruge sisi watanzania kwani nchi yetu inasifiwa kila
kona kwa kuwa na amani hivyo tunapaswa tuakikishe kuwa tunaendelea
kudumisha amani yetu sisi wananchi pamoja na nchi yetu kwa ujuma.
Aliwapa
pole wananchi wate wa mkoa wa Arusha kwa tatizo hili pamoja na majeruhi
wote ambao wameathiriwa na tatizo hili pamoja na wale wote ambao
wamepoteza ndugu zao kutokana na tatizo hili huku akiwashukuru
madaktari wote wale ambao wamewasiadia kuwaguza wagonjwa hawa na kuwasihi waendelee kuwaudumia vyema hadi pale ambapo watapona .
kwa
upande wa mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa mulongo alisema kuwa mpaka
kufikia leo asubui idadi ya marehemu imeongezeka na kufikia watatu
ambapo kijana mmoja ambaye akumtaja jina mwenye umri wa miaka saba
alifariki dunia leo asubui.