Mbali
ya serikali kuendelea kuchukua hatua ya kupunguza kasi ya tembo kuuwawa
kutoka tembo 55,000 kwa miaka ya sitini hadi tembo 110,000 kwa mwaka
2009,waziri wa maliasili na utalii balozi Khamis Kagasheki amevishukia
vyombo la ulinzi katika bandari kuu ya Dar es Salaam kuwa inatisha kwa
rushwa .
Waziri
Kagasheki ametoa kauli hiyo leokatika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini
Iringa wakati akifungua warsha ya siku tatu iliyoanza jana kwa wahariri
wa vyombo vya habari Tanzania .
Alisema
kuwa inashangaza kuona kontena na meno ya tembo linakamatwa nchi ya
Tanzania kwa kupitia bandari ya Dar es Salaam bandari ambayo kimsingi
idara zote za ulinzi zinapatikana katika bandari hiyo .
“Tunalilitetea
vipi kontena la meno ya Tembo….huku tukiambiwa na wakamataji kuwa
orijino yake ni bandari ya Dar e s Salaam bandari ambayo imetawaliwa na
polisi , TRA na watu wa usalama wa kada mbali mbali sasa limepitaje
nasema rushwa ndio inayoendelea kumaliza hifadhi zetu Tanzania hivyo
tusaidiane ili vizazi vijavyo visituhukumu kwa yale tunayotenda” alisema
waziri Kagasheki
“Lazima
tuwe na majibu kwanini, tusaidieni, kupunguza ujangili unaosababishwa
na mambo mbalimbali, rushwa ndani ya Mahakam, serikali na polisi
wamechangia kupungua kwa tembo”
Hata
hivyo alisema kuwa mchango mkubwa uko miongoni wanahabari wakiwemo
wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari katika kusaidia
kupiga vita vitendo vya ujangili ikiwa ni pamoja na kukemea rushwa,
maadili pia tama za watu wamefika mahali wanataka kufanya lolote lile
ili kutimiza matakwa yao.
Waziri Kagasheki alisema kuwa kwa kawaida watalii huvitiwa sana
kumuona tembo japo tafiti zinaonesha kuwa ujangili na uharibifu wa
mazingira umechangia kupungua kwa tembo katika hifadhi zetu .
Alisema
kuwa mwaka 1930 Tanzania kulikuwa na tembo milioni 50 wakati kwa sasa
kuna tembo 402,067 tu hali ambayo inaonyesha ni kwa kiasi gani tembo
wamepungua.
“Wahariri
jaribu kutafakari hilo tuendako si kuzuri Tanzania ni nchi ya pili
Botwasan ina tembo 154, 658 wakati Tanzania tunapoteza tembo wetu idadi
imepungua kutoka 250,000 na 300,000 katika miaka ya sitini hadi 55,000
katika miaka ya 1980”
Alisema
kuwa baada ya serikali kuchukua hatua sasa tembo 130,00 mwaka 20002 na
mwaka 2006 tembo 141,000 wakati takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2009
imepungua hadi 110,000 kwa mujibu wa takwimu za ujangili .
“Mnatakiwa
kuepuka vitu hivi tunajua kuna risks, lazima wawepo watu wa kujitolea
wenye uzalendo na uchungu wa taifa lao…. Vyombo vya habari vinaweza
kuifanya kazi hiyo”
Alisema
kuwa ujangili huo sit u kwamba unahatarisha kupotea kwa tembo, lakini
unaathiri utalii kwa ujumla wake hali hiyo inaashiria kutokuwepo kwa
amani hifadhinina uchumi wa nchi kwa ujumla.
Hakuna jinsi huko tunakokwenda, ujangili unaathiri kwa kiasi kikubwa utalii na pato la taifa asilimia 17.
“Hivi
sasa West africa hakuna tena wanyama, ivory coast ilikuwa kinara wa
kusafirsiha tembo, leo hawana kitu tusione haya muda umekwenda kama
tunataka kuzungumzia maslai ya nchini tusemezane ukweli”
Alisema
kuwa ili kukabiliana na mtandao mkubwa ujangili wa ndani ya nchi
unaotumia silaha za kisasa ni lazima kujizatiti na njama hizo
zinazotishia kupotea kwa tembo katika uso wa dunia,
Kwani
litakuwa jambo la kusikitisha vizazi vijavyo vikianza kusimuliana
kwamba kulikuwa na wanyama wakubwa wanaitwa tembo iwapo wadau kwa pamoja
kwa sasa hatutaungana kupambana na wahujumu hao wa hifadhi zetu .
“Vyombo
vya habari vina wajibu wa kuhakikisha ujangili unaondoka, msaada wenu
ni muhimu, onesheni kwa vitendo, to focus kwenye issue ili mamlaka
zinazohusika zichukue hatua”
Hata
hivyo alisema kuwa Serikali ipo tayari kupokea maoni ya wanahabari
katika shughuli hii ya uhifadhi ikiwa ni pamoja na yeye kama waziri
kujiwekea utaratibu wa kukutana na vyombo vya habari mara moja kila
mwezi ili kutoa taarifa zaidi zinazohusiana na mikakati hiyo na masuala
mengine yanayohusu wizara.
Kwa
upande wake mwenyekiti kamati bunge ardhi mazingira na maliasili James
Limbeli alisema kuwa ni vema mwandishi wa habari akafa kwa kutetea
taaluma yako, mambo ya msingi yenye tija kwa nchi. Kwa Tanzania kwa
kuwafichua wanaoua tembo ambao ni laslimali ya Taifa .
“Wanaendesha
biashara ya ujangili wanapesa, na inahusisha pia viongozi. …Wahariri
zipeni nafasi stori zinazohusu ujangili zisomeni kwa macho mawili”
Hata
hivyo alisema takwimu ya ujangili dhidi ya tembo zilizotolewa na waziri
Kagasheki kwa upande wake haziamini kwa sababu wanaoziandaa ni
watumishi wa serikali na wanafanya hivyo kulinda hadhi ya serikali.
“Takwimu
ni za wale wa hifadhi, katika maeneo nje ya hifadhi hali ni mbaya zaidi
hakuna bajeti, watumishi wachache na hakuna motisha kwa wale wachache
hivyo wanaandaa takwimu bora mradi ili kumfurahisha waziri japo sina
shaka na utendaji kazi mzuri wa waziri Kagasheki ”.
Alisema
kuwa taarifa za kuuwawa kwa tembo ambazo waziri Kagasheki anazo ni zile
zinazoandaliwa na wahifadhi ambao hata hivyo wanaziandaa ndani ya
hifadhi ila wameacha nje ya hifadhi na kuwa idadi ya tembo kuuwawa ni
kubwa zaidi ya ile ambayo serikali inayo.
Hata
hivyo Lembeli aliwataka wahariri kuwa na forum yao ya big five, ili
kusaidia suala la utalii ambayo ni sekta pekee inayoweza kulinusuru
taifa kiuchumi
“Nawaombeni
sana tusikubali ujangili kuendelea kupukutisha hifadhi zetu ……
Serengeti inaingiza zaidi ya sh bilioni 30 kila mwaka sasa iwapo
tutaacha iteketezwe na majangili fedha hizi tutazipata wapi”
Awali
waziri kivuli wa maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa alishauri
kuwepo kwa umuhimu wa kutunza rasilimali hizo kwa kuhubiri uadilifu.
Pia
alisema kuwa warsha kama hizo ni nzuri iwapo zitahusisha wadau wote
wanaozunguka hifadhi hizo kama sehemu ya kuweka nguvu ya pamoja katika
kuzilinda.
Mchungaji
Msigwa alisema kuwa kinachochangia ujangili ni kutona na watu kukosa
uzalendo kwani hivi sasa sehemu kubwa ya watu waliopewa kusimamia sheria
hawajui chochote .
Chanzo:Francisgodwinblog