ALBERT MANGWEA.
P-FUN.
MKURUGENZI wa Studio ya Bongo
Records, P-Funk, ‘Majani’ amewajia juu watu wanaotaka kujinufaisha na
msiba wa Albert Mangwair, huku akiw
alaani vikali wanaotumia msiba huo kujipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa zisizo sahihi.
Majani alisema hayo kufutia kuenea kwa
taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha picha ya msanii huyo
akiwa amepasuliwa tumbo na kukutwa na pipi za madawa ya kulevya wakati
akifanyiwa upasuaji.
Majani amesema kwamba taarifa kwamba alikutwa na pipi za madawa ya kulevya si za kweli kwa kuwa hakuna aliyethibitisha hilo.
“Kuna vitu vingi vya kuwafanya wawe
maarufu, lakini siyo kufanya vitu vya kudhalilisha maiti kwani ni maonyo
ya dini zote, ina maana watu wamemsahau Mungu kiasi hicho hadi kufanya
mambo yasiyoeleweka inashangaza sana, kibaya zaidi kuna baadhi ya watu
wapo huko kwa miaka mingi tunawaamini na wao wameingia kwenye mkumbo huo
wa kutoa habari zisizo na uhakika,”alisema Majani kwa hasira.
Majani alisisitiza kwamba kuna baadhi ya
mambo yanapaswa kuachiwa familia na endapo familia yake itahitaji msaada
watoe kadiri wanavyoweza.
Alisema hakuna sababu ya mtu au watu kujinufaisha kwa kifo cha
Mangwair ambaye alitumia nusu ya uhai wake kuitangaza nchi kupitia
muziki.