Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Tuesday, June 4, 2013

P FUNK ACHANGANYIKIWA KUONA JENEZA LA MANGWEA.

Editruda Mashimi,Dar es Salaam 
MWANDAAJI wa ala za muziki nchini Tanzania  P Funk Majani alichanganyikiwa baada ya kuona jeneza iliyokuwa imebeba mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.P Funk ambaye muda wote alikuwa amekaa kwenye gari akiwa na huzuni mkubwa kufuatia kifo cha msanii huyo, alibadilika ghafla baada ya kuona jeneza hilo likiingiz
wa katika gari maalum tayari kwa ajili ya safari kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.P Funk alishindwa kujizuia na akalazimika kushuka kwenye gari lake na kwenda kusukuma gari lililokuwa limebeba mwili wa msanii huyo aliyefariki Dunia Mei 28 mwaka nchini Afrika Kusini.
Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakazi wa jiji la Dar es Salaam kesho watapata fulsa ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la marehemu Mangwea katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mjini Morogoro kwa mazishi kesho kutwa.
http:/www.habrimpya.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...