Wakati huko bungeni Dodoma alhamis ya leo kulikuwa na maswali ya pako kwa papo kwa waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, upande wa mtandao wa kijamii wa twitter kuna maswali ya papo kwa papo kwa rapper wa Tamaduni Music Nikki Mbishi a.k.a Terabyte.
‘Playboy hitmaker’ ameamka na mzuka wa kujibu maswali ya fans wake tena bila kuchagua aina ya swali, “Leo nataka kuulizwa maswali tu na nitajibu yote.”
Katika kujibu maswali ya fans hao Nikki amelijibu swali la mtu mmoja aliyetaka kujua kama bado ana beef na msanii mwenzake ‘Ney wa Mitego’, “@nikkizohan #AskZohan Samahani lkn, Et mkuu Beef la ww na #NeyWamitego bado lipo au limekwisha tayali???”
Nikki akatoa jibu pana zaidi, “@AlmasMzambeleHB sina beef na msanii yeyote duniani!”
Jibu la swali hili liliibua swali jingine, nadhani ni kwa sababu Nikki Mbishi aliwahi kuwa na mtafaruku na wasanii wa kundi la Weusi akiwemo Bonta a.k.a Maarifa na Nikk wa pili.
Shabiki mmoja alimtupia swali kwa tweet hii, “@NikkiZohan @FidQ @yonnerpaul @Profesa_Jay zohan..vp huna mpango wa kufanya ngoma na member yeyote wa weuc kma unao ni nan utakaye fanya nae.”
Na hili ni jibu toka kwa freestyler baba Malcom, “@IamSindato @FidQ @yonnerpaul @Profesa_Jay tukiwa tayari nitafanya na yeyote atakayefit ngoma tutakayofanya.”
Hii inamaanisha yeyote kati ya Joh Makini, Nikki wa Pili, Bonta, Lord Eyez na G-Nako, hii pia inaweza kutafsiriwa kuwa amefuta tofauti iliyokuwepo kati yake na Bonta ama Nikk wa Pili.
Kwa upande mwingine, Nikki ambae amesema kila siku asubuhi huandika wimbo mmoja isipokuwa siku ambazo anapata dharura,Amelia na baadhi ya mashabiki wa hip hop kuwa sio die hard fans na kwamba endapo wangekuwa kama wale wa soka ingewapa wasanii wanaofanya Hip Hop ari zaidi.
“@hamrash87 mashabiki wengi sio die hard fans,wangekuwa wanashabikia hip hop kama soka ingetupa ari kubwa ya kuwapa mavitu ya hatari!”
Wengi hudhani wasanii wote wa Hip Hop hawapendi aina nyingine za muziki kama taarabu, bolingo n.k, lakini hii ni tofauti kwa Nikki Mbishi ambae yeye hachagui aina ya Muziki, yeye anapenda muziki mzuri ‘just good music’.
“@mark_wiwi kitu kinachoitwa muziki mi nakipenda haijalishi ni wa aina gani,just good music!” Alitweet Nikki Mbishi akijibu swali la Mark Wiwi aliyetaka kujua aina nyingine ya muzkiki anayoipenda mbali na Hip Hop.
Haya ni baadhi tu ya maswali na majibu, bado Nikki anaendelea kutoa majibu kwa fans wake.