Taarifa
ya Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa Rais wa zamani wa Taifa hilo,
bwana Nelson Mandela amepelekwa hospitalini alfajiri ya siku ya leo,
Jumamosi, Juni 8, 2013 kwa matibabu ya maradhi ya mapafu yanayojirudia
rudia na kusabababisha hali yake kuendelea kudhoofu.