Msanii Masele
Habari
za uhakika ni kuwa muigizaji wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la
Masele cha Pombe ni mzima wa afya na hajafariki kama baadhi ya tetesi
zilivyoanza kuenea kwa kasi. Pamoja blog baada ya kusikia tetesi kuwa
Masele amefariki kwa ajali ya gari jioni hii huko Tanga ilibidi kutafuta
ukweli kuhusu muigizaji huyo maarufu na kufanikiwa kupata habari za
kina kupitia Kabuti Onyango ambaye ni cameraman maarufu wa filamu za
kitanzania.
Kabuti
ambaye ni mtoto wa Mzee Onyango ambaye ni muigizaji mkongwe nchini
amesema kuwa amezungumza na baba yake(Mzee Onyango) muda mfupi uliopita
ambaye yupo Tanga na jibu ni hili " baba yupo Tanga mzee onyango na nime
mpigia simu kaniambia kwamba walikuwa na Masele kwenye hilo gari lakini
si kwamba amefariki hapana ila masele aligonga mtu akakamatwa na raia
wakavunja kioo na kutaka kumuua aligonga mtu wa kwanza na akataka
kukimbia akagonga mwingine ndio ilivyo kuwa lakini ni mzima na yupo
kituo cha police"