Kutokana
na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima
mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati
mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Mwanamuziki
Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa
na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo
alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yakekuna jina la Jay Dee.Tofauti
na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA
aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya
mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.
Mwana FA
alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika
katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana
na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana,
hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida
inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali
shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa
nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa
wamefika walikuwa kama 250 tu.