Rasmi
 darajani, amesisitiza hajawahi kuwa na bifu na Abramovich, ataka 
kumrejesha John Terry uwanjani, awataka wachezaji kucheza kwa uzalendo 
mkubwa.
Kocha
 aliyejaliwa  kuwa na maneno mia kidogo, Mreno Jose Mourinho leo hii 
ametambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa wazee wa darajani, klabu ya 
Chelsea.
Akizungumza
 na waandishi wa habari, Mourinho ambaye miaka ya nyuma akiwa na Chelsea
 alikuwa anajiita “The Speacial one” kwa tafsiri isiyo rasmi,  
akimaanisha mtu maalumu, leo hii ametoa kali ya mwaka baada ya kubadili 
jina hilo na kujiita “The Happy One” kwa tafsiri isiyo rasmi unaweza 
kusema “Mtu mwenye furaha pekee”.
Mreno
 huyo ambaye ametokea klabu ya Real Madridi ya Hispania leo mchana 
ametambulishwa jijini London na kujibu maswali mengi kutoka kwa 
wanahabari waliohitaji kujua mambo mengi kutoka kwake likiwemo suala la 
uhusiano na bosi wake Abramovich.
Mourinho
 ambaye miaka ya nyuma alitimuliwa na mmiliki wa klabu hiyo Roman 
Abramovich baada ya kushindwa kuelewana, leo hii amesema kipindi cha 
nyuma alikuwa na mahusiano mazuri na bosi wake, endapo wangekuwa na 
mahusiano mabaya asingerejea kwa mara ya pili darajani.
Akiongea na wanahabari wapatao 250 leo katika uwanja wa Stamford
 Bridge, aliulizwa kama ataendelea kujiita “The Special one”, kocha huyo
 mwenye umri wa miaka 50 kwa sasa alisema “I am the Happy One” na 
kumalizia maneno yake kwa kusema “nina furaha sana”.
Mourinho
 alisema ” Mambo mengi sana yametokea katika maisha yangu ya kufundisha 
soka na kazi yangu miaka tisa iliyopita, lakini ni mtu yule yule, nina 
moyo uleule, nina hisia zile zile za kupenda mpira na kazi yangu, lakini
 kwa sasa ni mtu mwingine kabisa baada ya kurudi nyumbani Chelsea, nina 
furaha sana”.
Mourinho
 amewataka wachezaji wake kujituma zaidi na kuongeza kuwa klabu ni 
muhimu kuliko wao, kwani isingekuwepo wao pia wasingekuwepo.
Credit: Pamoja Blog 
 
 




 
 
 
