Vyama vya wafanyikazi nchini Ugiriki vimeitisha mgomo wa masaa 24 ili
kupinga hatua ya serikali kufunga shirika la utangazaji la serikali la
ERT kama hatua ya kupunguza matumizi.
Waandamanaji wakipeperusha bendera nje ya makao makuu ya Televisheni ya Taifa, ERT wakipinga kufungwa kwa televisheni hiyo.
Uchaguzi wa mapema vyombo vya habari vya Ugiriki vimezungumzia kuhusu matarajio ya uchaguzi wa mapema, wakionya kuwa safari hii Samaras angeweza kusukuma washirika wa muungano mbali sana.
Wasosholisti na chama cha wachache cha mrengo wa kushoto wanaounga mkono serikali hiyo ya Ugiriki tayari wanakumbwa na shinikizo la ndani juu ya hatua kali zisizo maarufu, Ugiriki imekuwa ikitumia kwa kipindi cha miaka minne.
Gazeti la Kathimerini daily la kiliberali la Ugiriki limesema suluhu ipatikane kwa kipindi cha wiki moja au kuwe na uchaguzi huku gazeti la mrengo wa kati likizungumzia kuhusu michezo hatari ya sarakasi.
“Iwapo kutakuwa na hali ya kutoafikiana, mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi wa mapema yatakuwa na nguvu zaidi,” lilisema Kathimerini.
Samaras alionekana kuchukua hatua ya nyuma hapo jana, baada ya wasosholisti na vyama vya wachache vya mrengo wa kushoto vinavyounga mkono muungano wa serikali, kusema hatua hiyo ya kufunga shirika la ERT ni hatua isiyokubalika.
Wafanyakazi wa ERT wameendelea kutangaza habari za moja kwa moja kupitia mtandao wa intaneti asubuhi ya leo.
Hapo awali Samaras alitetea hatua ya kufunga shirika hilo, akisema wanaondoa matumizi yasio hitajika na kwamba wanalinda maslahi ya umma.
Vituo vya runinga na radio vilizimika ghafla hapo jana, na takriban wafanyikazi 2,700 wa vituo hivyo walifutwa kazi kama hatua ya serikali ya muungano ya Ugiriki kupunguza matumizi.
Polisi wa kutuliza ghasia waliwekwa nje ya ofisi za ERT nchini kote ili kuzuwia uharibifu wowote kufuatia maandamano hayo ya leo.