Mhe Sugu |
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda |
BAADA ya kauli
yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo
Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita Bungeni kwa kutaka
Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph
Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu amemuomba radhi mhe Pinda na
watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia katika kuonyesha hisia zake
juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge
huyo machachari amenukuliwa akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na
kauli yake iliyodai kwamba Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama
Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi
nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio
langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."